`TUHUMA za Mbowe Kuhamamisha Mabilion ya Hela Kutoka Kwenye Accont yake Kwenda Nchi za Nje....CHADEMA Wazungumzia Tuhuma Hizo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekashangwazwa na tuhuma za uongo zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe za kuhamisha fedha katika akaunti za nje.

Akizungumza na waandishi wa habari  jana, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alieleza kuwa hakuna sheria inayomkataza mtu kutofanya biashara na kuhamisha fedha zake binafsi.

Akitaja vyombo hivyo alisema kuwa ni Magezeti ya Jambo Leo, Uhuru na Raia Tanzania ambayo alidai yana maslahi ya kisiasa kwani habari hiyo imeonekana kuhaririwa na mhariri mmoja kutokana na kutokuwa na uthibitisho wala ushahidi wa upande wa pili.

Mimi ni mwandishi mwenzenu, naifahamu taaluma hii, ukisoma habari hiyo utaona inafanana kwa kila mstari, nukta hadi koma, inaelekea iliandikwa na mwandishi mmoja na kusambazwa kimaslahi kwa magazeti yote matatu na wahariri wakapachika” alisema Makene.

Alisema kuwa mwenyekiti huyo ni mfanyabiahara wa kimataifa ambaye anafanya biashara zake halali nje na ndani ya nchi zinazojulikana na serikali.Alisema magazeti hayo yanaandika ili kuwaondoa wananchi kwenye ajenda kubwa ya Uchaguzi sababu chama cha Mapinduzi kimeelemewa.

Jana Magazeti matatu yaliandika kuwa Freeman Mbowe, anatuhumiwa kuhongwa ili kumpitisha Edward Lowassa, kuwa mgombea urais wa chama hicho, yakimtuhumu kufanya uhamisho wa mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Uhuru, Jambo Leo na Raia Tanzania yaliandika kuwa zilikuwa ni njama za Mbowe, kufanya uamuzi wake wa kumpitisha Lowassa kuwania urais pasipo kushindanishwa na mtu ndani ya chama chake na ndani ya muda mfupi, uamuzi unaodaiwa kukigawa chama hicho,

Magazeti hayo kwa pamoja yaliandika kuwa Mbowe anahamisha hela hizo wakati wagombea kupitia chama chake hawana hela.

Hata hivyo Makene alifafanua kuwa hakuna sera ya Chadema kutumia pesa za mtu binafsi na biashara zake kwa ajili ya kusaidia wagombea, isipokuwa hela zinazopatikana kutokana na ruzuku hutumika kwa shughuli za chama na hesabu zake zinajulikana.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad