Chadema kwa kushirikiana na vyama vinavyounda Ukawa, leo wanakutana kujadili mwenendo waliouita usio halali wa kutangaza matokeo, wakiituhumu Tume ya Uchaguzi (NEC), CCM na Jeshi la Polisi kushirikiana kuhujumu matokeo.
Viongozi hao wa Ukawa, Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, James Mbatia (mwenyekiti, NCCR Mageuzi) na Profesa Abdallah Safari, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema walizungumza na waandishi wa habari jana Makumbusho jijini Dar es Salaam na kusema hawayatambui matokeo hayo kwa kuwa yamechakachuliwa.
Mbowe aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kuna vijana kutoka Kenya, ambao wamewekwa hoteli mmoja Dar es Salaam ambao wanafanya kazi ya kuchakachua matokeo yanayotoka majimboni na baadaye kuyapeleka NEC.
“Ndio maana matokeo yaliyopo kwenye fomu za mawakala wetu yanatofautiana na matokeo yanayotangazwa na NEC,” alisema mwenyekiti huyo wa Chadema.
Aliyataja baadhi ya majimbo hayo kuwa ni Nyamagana, Rungwe, Kahama Mjini, Shinyanga Mjini, Kyela na Muleba Kusini.
“Kazi hii ya uchakachuaji matokeo inafanywa na CCM, inaratibiwa na NEC na wasimamizi wakubwa ni polisi,” alisema Mbowe.
Akichangia suala hilo, Profesa Safari alitoa mfano wa Jimbo la Tandahimba ambako alisema NEC ilitangaza kuwa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli alipata kura 49,098 na Lowassa kura 46,288 ambazo ni tofauti ya kura 280.
“Lakini matokeo halisi kutoka kwa mawakala wetu yanaonyesha Lowasa alipata kura 44,537 na Dk Magufuli 44,253 ambazo ni tofauti ya kura 284,” alisema Profesa Safari.
Pia alisema NEC ilitangaza kuwa Lowassa alipata kura 6,000 Jimbo la Tunduma, wakati matokeo yao yanaonyesha alipata kura 32,442.
Mbowe pia alizungumzia vijana 191 waliokamatwa na polisi, ambao nane kati yao walifikishwa mahakamani jana kujibu mashtaka ya kufanya makosa ya kimtandao.
“Kitendo kilichofanywa cha kuwanyima dhamana ni cha kinyama hakistahili,” alisema Mbowe.
“Kwanza kuna wageni wawili ambao hawahusiki kabisa na shughuli za ujumlishaji matokeo ya Chadema.”
Alisema kitendo cha polisi kuwakamata vijana hao waliokuwa wakijumlisha matokeo, kimevuruga mfumo wa ukusanyaji matokeo wa Chadema.
“Lakini sasa tunatumia fomu za mawakala wetu ambazo zinaonyesha (mgombea urais wa Chadema, Edward) Lowassa anaongoza kwa tofauti kubwa ya kura,” alisema Mbowe.
Alisema vijana hao wamekamatwa kwa kosa ambalo linafanywa na mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ambaye Mbowe alisema amekuwa anatangaza matokeo ya uchaguzi na idadi ya majimbo bila ya kuchukuliwa hatua zozote.
“Huu si uchaguzi, ni uchafuzi,” alisema Mbowe.
Hata hivyo, Makamba alisema jana kuwa hakuna tatizo la yeye kusema kuwa watashinda kwa asilimia fulani kwa sababu kila chama kimekuwa kikisema hivyo.
“Hali hii inatufanya tuamini sababu za NEC kuchelewesha Daftari la Wapigakura na kutoruhusu wapinzani kukagua mfumo wa kujumlisha matokeo.”
Mbowe alisema wanalazimika kujadili sasa suala hilo kwa kuwa katiba hairuhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani.
Alisema Kamati Kuu ya Chadema inakutana leo jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo na kutoa tamko na pia kikao cha viongozi wa Ukawa kitakutana leo kutoa mwelekeo wa uchaguzi.
Akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi, Mbatia alisema: “Hili ni janga la Taifa linalotengenezwa na binadamu huku wakijua athari zake.
“Nchi ni mali ya watu wote na ukawa hawataki machafuko. NEC ikiendelea inaweza kukamilisha ile kauli kwamba uchaguzi wa mwaka huu utakuwa si huru.”
“Unaweza kuchakua matokeo lakini huwezi kuchakachua hisia za Watanzania,” alisema Mbatia.
Alisema kinachotokea ni kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kukataa mapendekezo ya vyama vya upinzani waliomtaka abadili mambo manne kwenye katiba kabla ya uchaguzi.
Aliyataja mamnbo hayo kuwa ni matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani, kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, mgombea urais ashinde kwa zaidi ya asilimia 50 na tume ya uchaguzi kuwa huru.
UKAWA Waja na Mpya Wasema Hawayatambui Matokeo ya Urais Yanayotangazwa na NEC
10
October 28, 2015
Tags
Makamba ni Jasusi. Hana Moyo, Wala hajijui. Amepagawa na nguvu za Mauaji, Kishetani.
ReplyDeleteNguvu za kiutamaduni, Kichawi. Inabidi mchawi mwenzake amwengue. Ndipo atajuta. Ni shetani mkubwa.
Mbowe manake hata jimboni kwako ulikoshinda NEC wamechakachua ili ushinde? usipande mbegu za chuki kwa watanzania, Siasa za chuki hazina nafasi. Ni heri makengeza ya macho uliyonayo kuliko makengeza ya uchu wa madaraka.
ReplyDeleteUtumbo utumbo. Hapa kwa nini unawasemea Wanawake. Wanawake sasa ni shujaa. Umemuona Mdee huna akili.
DeleteMbowe ww ni kibaraka tu huna lolote nenda kwenu ukalime mpumbavu
ReplyDeleteMpumbavu ni wewe usiye an elimu. ni mjinga kupindukia. Hata ukimkamata mwizi kwa vile hazimo juu utamweka awe mpenzi wako. atakuburuta na kukuchakaza sababu huna elimu. Ni vijana wa sasa na elimu za kata.
DeleteTunarudia kote inchi nzima asante mallimu seifu umeumbika watanganyika Na wanzibari
ReplyDeleteMbowe hana la
ReplyDeleteke kauza chama na sasa analalamika
Nyinyi Wajinga ndio mnalaza akili na elimu zenu duni mashindwa kujua haki zenu. Ni ujinga kupindukia. Ungejua nini mbowe anatetea ungeufyata. Ujinga ni sumu ya maendeleo. Sababu wajinga hawajijui kama ni wajinga. Ni kubweta tu.
DeleteUpumbavu ndio huu. Chama kimeboreka. Na kutokana na elimu na busara za mbowe na Wanaukawa sasa Tanzania na Watanzania wenye akili wanatambua jinsi CCM walivyo . Ni manyampala, wanynyasaji na wezi wa mali zaumma. Wameiba kura Zanzibar na Bara. Wamezoea wizi na za mwizi ni arobaini. Je Maraisi na Mawaziri husika hamna haya> hata wanafunzi wameshuhudia wizi wenu. Kwa maana hiyo mmepoteza mwongozo.
DeleteNyinyi mnaomsema mbowe wote si wajinga tu hamna elimu kabisa. Nawe wa kutoka ruvuma ambako kwa miaka yote hana maendeleo, mmelala bado hamna mwamko na mnawapigia CCM hata mkimwona Ridhiwa anawaibia madini. Ni wajinga kupindukia. Madini ya Mkaa lwanda yanachimbea kwenda China nyonyi hata maji safi hamna. Ni madini ya kwenu lakini hamjasoma wala hamjui haki zenu. Ni wajinga kama nyinyi mnaochangia na kuwaruhusu CCM wawachezee. Sababu majuu kwenu akili shida. Mkijipatia kigauni mnaringa sababu hamjui maendeleo na uhuru ni nini. Wangekuwa watu shujaa thelathini wenye msimamo kama mbowe Tanzania ingebadilika sana.
ReplyDeleteAkili mali. Kosa kila kitu pata akili.