Uliokuwa uongozi wa Young Dee watoa ofa ya video moja kwa kundi alilojitoa la Mtu Chee

Baada ya uongozi wa Million Dollar Boys (MDB) uliokuwa ukimsimamia Young Dee kusitisha kufanya kazi na rapper huyo, CEO wa kampuni hiyo na studio za Authentic, Millian ametoa ofa ya video kwa kundi la Mtu Chee ambalo Young Dee pia amejitoa.
mtu chee
Kundi la Mtu Chee lililoanzishwa na rappers Stamina, Country Boy na Young Dee, leo wameachia single mpya bila Young Dee huku wakiwa wamemwongeza Young Killer kwenye single hiyo.
Young Dee alikaririwa hivi karibuni akidai kuwa uongozi wake (MDB) ulimzuia kuendelea kuwa member wa kundi hilo.
Millian amethibitisha kutohusika katika maamuzi ya Young Dee kujiondoa Mtu Chee, kwa kujitolea kuwapa ofa ya video ya wimbo mmoja kundi hilo.
Kupitia post ya Instagram ya Country Boy, Millian alicomment kwa kuandika;
“Natoa offa ya kuwafanyia music video yenu moja bure wanangu. Dee farasi sana alivyosema Eti management yake imemzuia kufanya Kazi Na nyie @countryboytz @youngkillermsodoki @staminashorwebwenzi”
Country boy alijibu;
“thanx bro tunapokea na tunajua umuhimu wako kaka mkubwa Asante tupo tayari”
maxi na mtu chee
Source:Bongo5
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad