UPDATES za Matokeo ya Urais..John Magufuli Aendelea Kumgaragaza Edward Lowassa..Sasa CCM Inaongeza Majimbo 17

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Usiku huu imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 27 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo 17 wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo 10.

Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa awamu tatu, ambapo asubuhi  mwenyekiti huyo alitangaza majimbo matatu ambayo ni  Paje, Makunduchi na Lulindi ambayo yote Dk Magufuli ameongoza.

Majira ya alasiri , Jaji Lubuva alitangaza majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo majimbo sita yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo manne yakionyesha Lowassa anaongoza.

Usiku  huu  majira  ya  saa  mbili , Jaji Lubuva ametangaza majimbo mengine 14 ambapo kati ya hayo majimbo 8 yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo 6 yakionyesha Lowassa anaongoza.

Majimbo hayo ni kama  ifuatavyo:
Matokeo ya Urais Singida Mjini
Kura: 56,558
Magufuli (CCM): 36,035
Edward Lowassa (Chadema): 19,007

Matokeo ya Urais Jimbo la Lindi Mjini
Kura: 38,992
Magufuli (CCM): 21,088
Edward Lowassa(Chadema): 17,607

Matokeo ya Urais Jimbo la Njombe Mjini
Kura: 55,772
Magufuli (CCM): 33,626
Edward Lowassa(Chadema):20,368

Matokeo ya Urais Jimbo la Peramiho
Kura:45,374
Magufuli (CCM): 32,505
Edward Lowassa (Chadema): 11,291

Matokeo ya Urais Jimbo la Mkinga
Kura: 39,788
Magufuli (CCM): 23,798
Edward Lowassa (Chadema): 15,142

Matokeo ya Urais Jimbo la Moshi Mjini
Kura:79,814
Magufuli (CCM): 28,909
Edward Lowassa (Chadema): 49,379

Matokeo ya Urais Jimbo la Nanyamba
Kura: 44,437
Magufuli (CCM): 24,904
Edward Lowassa (Chadema): 16,992

Matokeo ya Urais Jimbo la Mbinga Mjini
Kura: 42,717
Magufuli (CCM): 29,295
Edward Lowassa (Chadema):11,695

Matokeo ya Urais Jimbo la Kisarawe
Kura: 38,012
Magufuli (CCM): 24,086
Edward Lowassa (Chadema): 13,093

Matokeo ya Urais Jimbo la Mgogoni
Kura: 7,539
Magufuli(CCM):710
Edward Lowassa (Chadema): 6,506

Matokeo ya Urais Jimbo la Mtambwe
Kura: 7,620
Magufuli (CCM): 428
Edward Lowassa (Chadema): 6,937

URAIS Jimbo la Kojani
CCM - kura 1561
CHADEMA - kura 9982

URAIS Jimbo la Wete
CCM - kura 958
CHADEMA - kura 5119

URAIS Jimbo la Gando
CCM - kura 881
CHADEMA - kura 5903
10. URAIS Jimbo la Lindi Mjini
Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa kesho  saa  tatu  asubuhi.

Top Post Ad

Below Post Ad