Karatasi hizo zilikuwa zimesambaa nyuma ya bweni la wanafunzi wa kidato cha sita, hali iliyowafanya wanafunzi wahisi kuwapo kwa karatasi zaidi ndani ya mabweni.
Mmoja wa wanafunzi alisema karatasi hizo zilisambaa nyuma ya bweni hilo baada ya mwanafunzi mmoja kuzirusha kupitia dirishani kutokana na kutuhumiwa kutumiwa na mmoja wa wagombea kwenye jimbo hilo lenye ushindani mkali kati ya Chadema na CCM.
Mmoja wa walimu, Charles Rushinge alisema aligundua karatasi hizo wakati akikagua mazingira ya shule na baadaye kutoa taarifa kwa vyombo husika kwa ajili ya kuchukua hatua.
Hata hivyo, pamoja na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi kufika shuleni hapo kushuhudia tukio akiwa na baadhi ya maofisa usalama, bado hakuwa tayari kutoa ufafanuzi wa idadi ya karatasi za kura na chanzo cha tukio hilo.
Tukio hilo liliibuka huku yakiwepo malalamiko mengi katika vituo vya Kata ya Kashai kuwa kuna karatasi zimenyofolewa kutoka kwenye baadhi ya vitabu vya kupigia kura, ikiwa ni pamoja na kituo cha Zahanati ya Kashai na Shule ya Msingi na Mafumbo.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Jimbo la Bukoba Mjini, Aron Kagurumjuri aliwataka wananchi wapige kura na kudai alipokea vitabu kutoka NEC vikiwa vimefungwa kwenye maboksi, hivyo tatizo la karatasi hizo za kura si lake....Tazama Video hiii