Wako Wapi Wabunge Washangiliaji wa Lowassa na Wenyeviti Watiifu Kwake?

Siku Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kulitaja jina la Edward Lowassa wabunge walilipuka kwa kushangilia na Bunge kuzizima. Rais Kikwete alikuwa akihitimisha miaka ya Bunge kuelekea kufanyika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Jina la Edward Lowassa lilitajwa wakati Rais Kikwete akiwataja Mawaziri wakuu aliofanya nao kazi na kuwashukuru.

Kulipuka kwa Bunge kulimaanisha kuwa Edward Lowassa alikuwa akiungwa mkono na wabunge wengi ambao wengi wao wanagombea tena. Lakini wengi wamebaki CCM baada ya Lowassa kuhamia CHADEMA. Kwakuwa wakati huo hata mchakato wa kura ndani ya CCM haukuwa tayari, nguvu ya Lowassa ilijidhihirisha hata mbele ya Rais Kikwete. Mara nyingine ilikuwa ni kule Dodoma wakati wimbo wa Lowassa ulipoimbwa baada ya kukatwa jina.

Pia, walijitokeza wenyeviti wa mikoa na hata makada kindakindaki wa CCM waliojipambanua kama wanaomuunga mkono Lowassa wakati akiwa CCM. Ingawa wapo waliojitoa CCM na kujiunga na CHADEMA kumfuata Lowassa, wabunge wengi waliomshangilia na wale wenyeviti waliomuunga mkono wamebaki CCM wakiwa kimya. Wako wapi waendelee kumuunga mkono chaguo lao? Nini kimempata Msukuma na Kangi Lugora? Ni waoga au bendera-fuata upepo? Waaminike?

By Petro E. Mselewa; JF

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waache wabaki huko ccm. Muhimu ni kura yao ya siri kwa Lowassa. Nape wala Makamba hawataona.

    ReplyDelete
  2. Ccm gar kubwa magufuli atashinda tena kwa kishindo

    ReplyDelete
  3. MSIMAMO WA WABUNGE HAWA WA CCM KUMUUNGA MKONO MHESHMIWA LOWASSA UPO PALE PALE TENA KWA NGUVU SANA JAPO HAWAKUMFUATA LOWASSA UKAWA-CHADEMA.NA HII INADHIHIRIKA KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU ZINAZOFIKIA TAMATI TAREHE 24 OCTOBA 2015.WANASEMA HIVI KWENYE KAMPENI ZAO"nichagueni mimi ili niendeleze na kukamilisha miradi mingi niliyoanzisha,na kwa upande wa mgombea urais LICHAGUENI JEMBE,MASHINE KUBWA,EDWARD LOWASSA" MANENO HAYA PEKE YAKE YANAHITAJI MOYO NA UJASIRI MKUBWA.CCM WANAJUA,NA,WAFANYE NINI,TAYARI NI WAGOMBEA WAO.PILI KUHAMA KWA WABUNGE HAO WA CCM EN-MASSE KUMFUATA MHESHIMIWA LOWASSA CHADEMA-UKAWA JAMBO HILI PRACTICALLY LISINGEWEZEKANA KUTOKANA NA MAMBO MAWILI.KWANZA IKUMBUKWE UAMUZI WA LOWASSA KUHAMIA CHADEMA ULICHUKULIWA WIKI YA MWISHO YA JULY 2015 WAKATI CCM ILIKWISHA MALIZA MCHAKATO WAKE WA KUWATEUA WAGOMBEA UBUNGE.PILI NDANI YA CHADEMA YENYEWE NI CHAMA KILICHOKWISHA KOMAA KISIASA,KIMEKAMILIKA KILA IDARA NA PIA KWAMBA TAYARI WAKATI ULE JULY MWISHO MCHAKATO WA KUTEUA WABUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA ULIKUA UKINGONI. KAMA EN-MASSE YA CCM INGETUA CHADEMA BASI PANGETOKEA SHIDA KUBWA BADALA YA NEEMA KUBWA.KUHAMA EN-MASSE KUNA CONSIDERATIONS NYINGI NA HUSUSANI SACRIFICE-PREPARDNESS.ILA SASA KUELEKEA 2020 .UPO MUDA WA KUTOSHA, NA,NAFASI YA KUTOSHA.MWISHO NIZUNGUMZIE KUHUSU BUNGE JIPYA LIJALO NOVEMBA 2015.HILI LITAKUA NI BUNGE LA MAPINDUZI MAKUBWA SANA LITAIPITIA UPYA MIKATABA MINGI TATA NA HARAMU ILI IJADIRIWE NA KUPITISHWA UPYA ,LITAREJESHA HESHIMA YA BUNGE.LITAKUA BUNGE LA LOWASSA AU LA UTAWALA WA LOWASSA.LEO NIISHIE HAPO.ZAIDI NITAWAPA BUNGE NA WABUNGE WAPYA TAREHE 10.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad