Wassira: Sikubalini na Matokeo ya Ester Bulaya....Nimehujumiwa

Stephen Wassira 
Saa chache baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kumtangaza Ester Bulaya wa Chadema kuwa mshindi katika jimbo la Bunda Mjini, aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo na mpinzani wake mkuu Stephen Wassira amejitokeza na kupinga matokeo hayo.


Wassira amedai kuwa matokeo hayo sio halali na kwamba kuna hujuma zimefanywa ili kumuangusha na kumpendelea Esther Bulaya.

Ester Bulaya Aliyemwangusha Wassira
Wassira ambaye pia alikuwa Waziri wa Chakula na Ushirika, amedai kuwa matokeo yaliyotangazwa yana kasoro kubwa ikiwa ni pamoja na idadi ya kura zinazoonekana kuwa zilipigwa zinazidi jumla iliyopo kwenye matokeo hayo.

Alisema kuwa msimamizi wa uchaguzi alimhujumu kwa kuongeza tarakimu kwenye matokeo hayo na kwamba tarakimu hizo zilipelekea idadi ya wapiga kura kwenye kituo kimoja kuzidi idadi iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mwanasiasa huyo mkongwe pia amedai kuwa msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo bila kuzingatia sheria ya uchaguzi.

Ester Bulaya na Wassira ni mahasimu wakubwa wa kisiasa ambao walianza ushindani mkubwa katika jimbo hilo tangu Ester Bulaya alipokuwa mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu wengine hata vioo Hawana
    Mtu mzima ovyo hata turudie mara 1000000000000000000000000000000000
    Wasira hupati ngo tena wabunge wateule wamefurahi sana Kwani ulikuwa kero kwa mkoromo wako bungeni
    Ndungai huwi spika ngoooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  2. Sasa wasira nae alalamike kuhujumiwa ntashindwa kuelewa, mzee wangu Wasira ndo maan ya uchagz -ve & +ve yote ni Majibu

    ReplyDelete
  3. Jamani dada wa watu kashinda kwa amani kabisa Wasira wananchi wako wa Bunda hawakutaki tena hata hivyo umekwishazeeka kapumzike na wajukuu zako nyumbani pole baba.

    ReplyDelete
  4. Unajuwa CCM kuna mizabwada kazi kupiga debe maisha yao yanategemea kauri zao Tanzania
    Wasira kifo cha mende Kama huna nyumba dar nunua hiyo hiyo ya serikali lakini bunda sahau

    ReplyDelete
  5. Babu kapumzike,pumzi imekata mbona?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad