Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM, Dr John Pombe Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.
Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr magufuli amepata ushindi wa kura Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45% huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu , Edward Lowassa (Chadema ) ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 ( 6,077,848 ) sawa na asilimia 39.97%
Dr Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi vyetu vya ushindi kesho saa nne asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya Diamond Jubilee
YAMETIMIA:Dr John Pombe Magufuli Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania kwa Asilimia 58.45
8
October 29, 2015
Wapi ukawa na moto wa mabua, chezea ccm weye
ReplyDeleteASANTE WALIOMPIGIA KURA MUHESHIMIWA MAGUFULI.MUNGU AWABARIKI MNO HASA PALE MLIPOTUMIA BUSARA BILA KUJALI UCHOCHEZI WA WAUME/WAZAZI.BINAFSI SIKUPIGA KURA KWA SABABU NILIKUWA NALAZIMISHWA NA MUME NIMPIGIE KURA LOWASA KWA KIAPO,SIKUWEZA NA NIKASEMA BORA NIACHE KUPIGA KURA,NILIOMBA MUNGU MAGUFURI ASHINDE NA KAJIBU MAOMBI.
ReplyDeleteHAPPY BIRTH DAY MR. PRESIDENT!!!
ReplyDeleteHongera sana wana CCM kwa chama kuongoza kwa mara nyingine tena.Ile HAPA KAZI TU na iwe kazi kweli tukimtanguliza Muumba wetu mbele.Tumeshinda ila cha moto tumekiona na tukilegea na kuchemka itakula kwetu.Hii ni TZ mpya.R.I.P UKAWA KARIBU ACT KWA MAPAMBANO.
ReplyDeleteShukrani za kipekee zimuendee Mzee wa Kubadilisha gia angani aka Mbowe, bila yeye kutuondolea lile 'zigo', CCM ingeonja joto ya jiwe. Kwa kweli kuna mchango wake mkubwa tu katika ushindi huu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni......THANK YOU MR. DJ!!!!
ReplyDeleteNi Rais wa Watanzania wote,ukubali ukatae ndio imekuwa.
ReplyDeleteWatanzania wengi tumemkubali,hata baadhi ya wapinzani pia,NI MCHAPAKAZI,na matunda tumeyaona,afya tele na push-up kwa sana tu tofauti na upande wa pili,lakini kumbe eti tatizo chama chake anachotoka,lakini kwani si chaguzi bado zinaendelea?akichemka tunampiga chini vilevile.Mungu ibariki TANZANIA.
Hongera DR.Magufuli, hongera watanzania kwa maamuzi sahihi. Tusibweteke tuchape kazi.Maendeleo hayaji kwa ahadi za jukwaani bali kwa kazi. "TANZANIA HAPA KAZI TU"
ReplyDeleteNa hiyo kauli mbiu ya hapa kazi itekelezwe watanzania WA Leo sio WAle wa tanu yajenga nchi, usipoleta tunalotarajia kweli tutakupiga chini muheshimiwa wetu, hongera Sana rais mpya tupe Tanzania mpya na ccm mpya sio ya kurithishana vizazi vya vigogo Tu, ccm iwe ya wote PIA futa ule msemo WA ccm Ina wenyewe, tumekupa nchi mtangulize Mungu
ReplyDelete