Agizo la Rais Magufuli kuhusu kununuliwa vitanda hospitali ya Muhimbili latekelezwa

Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge zipelekwe Katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya wagonjwa wanaolala chini limetekelezwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, Baiskeli za kubebea wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vinafungwa  jumapili na kwamba atakwenda kuvikagua siku ya jumatatu vikiwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokua wanakosa vitanda vya kulalia na kulazimika kulala chini.

Wadau mbalimbali walichanga fedha kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge baada ya uzinduzi rasmi wa bunge la 11 lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU,
Novemba 21, 2015.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. TAKE FIVE MR.PRESIDENT!SHOW THEM WHO WERE THERE BEFORE YOU BUSY WITHOUT NO SHAME AND CLEAN HEART 24HRS DAILY STEALING FROM POOR TANZANIANS HOW IT WAS SUPPOSED TO BE DONE AS A PRESIDENT!RESPECT MR.PRESIDENT GOD BLESS YOU

    ReplyDelete
  2. I salute you Mr. JPJM......HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad