Aunty Lulu Amchana Wastara Juma...Adai Akubali Yaishe Kwa Mr Bond

BAADA ya hivi karibuni wasanii wa filamu waliokuwa wapenzi, Wastara Juma na Bond Suleiman kutengana, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ameibuka na kumshauri staa huyo kukubaliana na matokeo.

Aunty Lulu aliyewahi kuwa mpenzi wa Bond, alimtaka mwenzake kukubaliana na matokeo kwani huenda muda ndiyo umefika na katika mapenzi, hilo ni jambo la kawaida.

Sina la kuzungumza juu ya Bond maana sihusiani naye, mapenzi yalikuwa zamani ila kama uchumba umevunjika basi namshauri Wastara akubaliane tu na matokeo kwani hata mimi muda wangu uliisha, tukaachana naye inawezekana ni hivyo umekwisha pia,” alisema Aunty Lulu.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad