Siku ya tatu baada ya Rais Dk Magufuli kuingia Ikulu na kuanza kazi alifanya ziara za kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni baada ya kumaliza ziara katika Wizara ya Fedha siku moja baada ya kuapishwa.
Baada ya kutembelea hospitali ya Muhimbili alifanya mabadiliko ikiwa kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Hussein Kidantu sambamba na kutaka mashine za CT Scan na MRI zifanyiwe ukarabati baada ya kukaa miezi miwili bila kuhudumia wagonjwa kutokana na ubovu wake.
Kamati mpya tendaji ya hospitali hiyo ilikutana jana na mara moja kuitisha wataalam ambao leo walianza kazi ya utengenezaji wa mashine hizo.
Taarifa mpya kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaisha amesema ni kweli mashine za MRI tayari zimeanza kufanya kazi na mashine za CT Scan bado zipo katika matengenezo na zitaanza kufanya kazi wakati wowote kuanzia sasa.
Barua ilisomeka hivi…
Baada ya Magufuli Kutembelea Muhimbili Kwa Kushtukiza..Hii ni Habari Mpya ya Kufurahisha Kuhusu Mashine ya MRI
2
November 11, 2015
Tags
kichwa cha mwendawazimu............... kwahiyo hata kutengeneza hivyo vipimio muhimbili vilikuwa vinasubiri ziara ya kushtukizwa au ndo hapa kazi tu linatumika ndivyo sivyo?? mnaangaika sana kutafuta sifa za kijinga.
ReplyDeletehovyo kabisa, wanasubiri mpaka watembelewe na rais ndiyo wafanye kazi, tena kwenye masuala ya afya, Mheshimiwa Raisi naomba uunde kamati maalum yakuwafuwatilia hawa watu wa afya, wakiboronga, siyo tu kuwafukuza kazi, wawekwe ndani, hii ni AIBU.
ReplyDelete