Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wamempigia kura na kumchagua tena mgombea ambae alishinda awali Omari Abdallah Kigoda katika uchaguzi uliofanyika wilayani humo leo baada ya kamati kuu ya CCM Taifa kutaka urudiwe.
Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti aliyesimamia uchaguzi huo Dk Maua Daftari alisema kuwa wajumbe wote kwenye mkutano walikuwa 690 na waliopiga kura ni 660 na uchaguzi ulikuwa wa wazi na haki na hakukuwa na tatizo lolote.
Alisema Omari Kigoda amepata kura 402 na mgombea mwenzake Hamisi Mnondwa alipata kura 257 huku kura moja ikiharibika na kufanya jumla ya kura zote kuwa ni 660 hivyo kumtangaza Omari kuwa mshindi katika kura halali 259.
Awali kabla ya uchaguzi huo mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Taifa Abdallah Bulembo alisema kuwa sababu kubwa ya kurudiwa uchaguzi huo ni kutokana na mshindi wa kwanza na aliyemfuatia kushindwa kuvuka nusu ya idadi ya wapiga kura hivyo hawakufika katika vigezo vinavyotakiwa.
Mgombea huyo anatarajiwa kwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Handeni Mjini kesho na kuirudisha ambapo tarehe tano wataanza kampeni rasmi.
ndo nchi yao hii kumamae tushachoka raia madaraka ya kisultani mpaka lini
ReplyDeleteChadema mtaishia kutukana tu, IKULU mtaliona GATE wakati mkienda ferry kununua samaki.
DeleteWe'chamatusi subiri usikie majina ya viti maalum ya chadema ndio 'utachekelea' Mery Mbowe, Magdalena Lowasa, Vicky Mtei, Joyce Lissu, Stela Mnyika, Rose Lema ha ha ha PpiiiiPooooooz PWAAAA!! Ahsanteni power mmempatia TINGATINGA..... NANI AMENUNA??????
Yes ndo CCM kula kwa kutesa hata aibu hawana
ReplyDeletewajane...... wa filikunjombe na wamtikila, na kigane wa celina,...
wote bungeni, hiyo ndo tanganyika
Jamaani mbona tuna hizo roho za korosho kwani huyo kijana karithishwa na familia yake mbona demokrasi imetendeka na kuchaguliwa na wanachama sasa ya usultani yanatoka wapi
ReplyDeleteUsishangae ndugu yangu, chadema wanatoa 'madukuduku' yao kupunguza 'msongo', wakibwabwaja kama hivyo kuna unafuu fulani wanaupata.........waache waseme mchana usiku watalala, kesho JPJM anakula kiapo cha URAIS.........NANI AMENUNA??????
DeleteKama baba yako hakuwahi kuwa waziri au mbunge usitegemee kushika nafasi yotote ya serekalini hii ndo TZ yetu
ReplyDeleteHivi ulipeleka maombi yako kugombea hapo jimboni ukakataliwa?
Deleteingia msituni
Delete