Breaking News: CCM Wampitisha Mtoto wa Marehemu Abdallah Kigoda Kuwania Ubunge Jimbo la Handeni Mjini

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM  wamempigia kura na kumchagua tena mgombea ambae alishinda awali Omari Abdallah Kigoda katika uchaguzi uliofanyika wilayani humo leo baada ya kamati kuu ya CCM Taifa kutaka urudiwe.

Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti aliyesimamia uchaguzi huo Dk Maua Daftari alisema kuwa wajumbe wote kwenye mkutano walikuwa 690 na waliopiga kura ni 660 na uchaguzi ulikuwa wa wazi na haki na hakukuwa na tatizo lolote.

Alisema Omari Kigoda amepata kura 402 na mgombea mwenzake Hamisi Mnondwa alipata kura 257 huku kura moja ikiharibika na kufanya jumla ya kura zote kuwa ni 660 hivyo kumtangaza Omari kuwa mshindi katika kura halali 259.

Awali kabla ya uchaguzi huo mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Taifa Abdallah Bulembo alisema kuwa sababu kubwa ya kurudiwa uchaguzi huo ni kutokana na mshindi wa kwanza na aliyemfuatia kushindwa kuvuka nusu ya idadi ya wapiga kura hivyo hawakufika katika vigezo vinavyotakiwa.
Mgombea huyo anatarajiwa kwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Handeni Mjini kesho na kuirudisha ambapo tarehe tano wataanza kampeni rasmi.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ndo nchi yao hii kumamae tushachoka raia madaraka ya kisultani mpaka lini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chadema mtaishia kutukana tu, IKULU mtaliona GATE wakati mkienda ferry kununua samaki.

      We'chamatusi subiri usikie majina ya viti maalum ya chadema ndio 'utachekelea' Mery Mbowe, Magdalena Lowasa, Vicky Mtei, Joyce Lissu, Stela Mnyika, Rose Lema ha ha ha PpiiiiPooooooz PWAAAA!! Ahsanteni power mmempatia TINGATINGA..... NANI AMENUNA??????

      Delete
  2. Yes ndo CCM kula kwa kutesa hata aibu hawana

    wajane...... wa filikunjombe na wamtikila, na kigane wa celina,...
    wote bungeni, hiyo ndo tanganyika

    ReplyDelete
  3. Jamaani mbona tuna hizo roho za korosho kwani huyo kijana karithishwa na familia yake mbona demokrasi imetendeka na kuchaguliwa na wanachama sasa ya usultani yanatoka wapi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usishangae ndugu yangu, chadema wanatoa 'madukuduku' yao kupunguza 'msongo', wakibwabwaja kama hivyo kuna unafuu fulani wanaupata.........waache waseme mchana usiku watalala, kesho JPJM anakula kiapo cha URAIS.........NANI AMENUNA??????

      Delete
  4. Kama baba yako hakuwahi kuwa waziri au mbunge usitegemee kushika nafasi yotote ya serekalini hii ndo TZ yetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi ulipeleka maombi yako kugombea hapo jimboni ukakataliwa?

      Delete
    2. ingia msituni

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad