Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia
Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni kushawishi watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini nyingine.
Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na hukumu hiyo.
Breaking News: Sheikh Issa Ponda Ashinda Kesi ya Uchochezi na Kuachiwa Huru
6
November 30, 2015
Woooooow
ReplyDeletePeople power rrrrrrrrrrrrrrrrrrr
MWENYEZI MUNGU MKUBWA, ALLAH AKULIPE UJIRA MWEMA KWA KUPATA MATESO KWA AJILI YA DINI YAKE. AMIN, TAKBIIIR!
ReplyDeleteM/Mungu atawashinda hao na Mtume s.a.w atawashindilia stahamili shehe wetu.
ReplyDeletemmmh.. jamaa kasota na kesi ya muda mrefu. pole usirudie tena mambo ya ubabe,, naamini mtume s.a.w alikuwa mpole japo simjui.
ReplyDeleteSheikh fundisha Dino sio ugaidi,hiki ni kisiwa cha Amani,ukitaka ugaidi nenda Syria .hapa kazi tu
ReplyDeleteikiwa ugaidi mbona ushahidi haupo, SHEIKH endelea na msimamo wako wa kuitetea dini hata hao Mitume walipata tabu sana na we unalijua hilo. ALLAHU AK-BAR.
ReplyDelete