Kamati Kuu CCM imewapitisha Job Ndugai, Abdullah Ali Mwinyi na Dr. Tulia Ackson Mwansasu kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la 11.
Majina hayo yamepenya kutoka katika orodha ya majina 21, miongoni mwao akiwemo Spika wa Bunge la 9, Samuel Sitta, Dkt. Didas Masaburi ambaye alitangaza kujitoa katika dakika za mwisho, Dkt Kalokola na wengineo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni ya leo baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichoongozwa na mwenyekiti wake Dkt Jakaya Kikwete mjini Dodoma, jina moja kati ya hayo matatu litatangazwa kesho Jumatatu ikiwa ni pamoja na jina la mgombea wa nafasi ya Naibu Spika.
Katika waliopitishwa:
Job Ndugai ni mbunge mteule jimbo la Kongwa Dodoma na pia alikuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita.
Dkt Tulia Ackson ni Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali, pia alikuwa ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akitokea taasisi za elimu ya juu. Amekuwa mhadhiri wa sheria katika kitivo (sasa shule) cha sheria chuo kikuu cha Dar es salaam.
Abdullah Mwinyi ni mtoto wa Rais mstaafu Al Hajj Aly Hassan Mwinyi na ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Tupeni job ndugai ndio anafaa pale bungeni
ReplyDeleteHakuna spika hapo
ReplyDeletewahi wahi mahakamani SAMWELI SITTA leo jumatatu tarehe 16 novemba 2015,wahi kama ulivyotishia.umepukutika kisiasa kwa aibu kubwa,tena kubwa sana.kwa kuwa wewe bado ni muhitaji wa siasa unaonaje sasa ukaanzisha chama chako kama ulivyothubutu wakati ule unaanzisha ccj.umejawa na uroho mkubwa na tamaa mbaya ya kujilimbikizia.ccm tunasema 'uende salama',nenda.
ReplyDeleteSpika mpeni mtoto wa Mwinyi Na uwaziri mkuu mpeni ridhwan Kikwete
ReplyDeleteTulia bomu alikuwa akipewa mitihani na majibu na dr migiro
ReplyDeleteChuo kikuu
Mzee sitta yuko chali,kapigwa ngumi ya utosi na ccm.kalegea sijui ni presha au ni sukari.huyu babu alishindwa kusoma nyakati.alitaka arejee bungeni kukumbana na nguvu mpya kali ya ukawa.walikua ukawa 86 bunge lililopita,sasa wapo 116,ongezeko la kutisha la wabunge wapya wa ukawa zaidi ya 40.wapo wapya hatari mno kama akina kubenea,lwakatare,bulaya,matiku na wengineo kibao,tele tele.bunge lingemshinda vibaya sana babu.ila yote kwa yote aliwahi kusema anastaafu siasa. najiuliza kichwa chake ni sawa?au mirembe referral.
ReplyDelete