Breaking News:UKAWA Wamtangaza Ole Medeye kuwa Mgombea Uspika..Sasa Kuchuana na Job Ndugai

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umemteua, Goodluck Ole Medeye (Chadema) kusimama katika nafasi ya uspika,huku katika nafasi ya unaibu Spika akiteuliwa,Magdalena Sakaya wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mwakilishi aliyekuwa anatazamiwa kuwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kinyang’anyiro cha nafasi ya uspika Mpekuzi ilibaini kuwa jina la Goodluck Ole Medeye, ndilo lililokuwa likitajwa kuwa litasimamishwa katika nafasi hiyo.

Ole Medeye, aliwahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi kupitia CCM,aliwahi pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete (CCM).

Umoja wa Vyama unaofahamika kama Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ndiyo sawasawa ole medeye na sakaya watapata kura zoooote,zote kabisa za ukawa yaani 116,na hicho ndicho kitakachokua kiashiria cha kwanza cha UKAWA SOLIDARITY kwa miaka mitano ijayo kabla ya uchaguzi mkuu ujao ukawa itakapochukua nchi.bunge la safari hii tamu.

    ReplyDelete
  2. ooh wow! Ole medeye the next speaker!

    ReplyDelete
  3. UKAWA HAWANA AKILI KAMA LOWASA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad