Breaking News:Waziri mkuu Majaliwa avamia bandari leo, aamrisha kukamatwa kwa maafisa kibao wa TRA

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.

Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.

Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. moto.ugali moto,mboga moto.

    ReplyDelete
  2. kweli hapa kazi tu

    ReplyDelete
  3. Asante Mungu,Maana kijana anaanza kazi bandari/TRA ndani ya mwaka mmoja ana nyumba 3 magari ya kifahari,heeeeeeeh kumbe jamani kuna watu wanatumia/wanaiba hela za uma kiasi hiki bila woga.mweeeh.funga wote na nyang'anya mali zao.TUMECHOKA.

    ReplyDelete
  4. Manina zao hao wezi wakubwa,kazi kuchezea dada zetu tu kuwanunulia magari na kuwapangishia majumba kwa hela za wizi.
    Na bado Mungu atawapiga makofi mpaka mjue kuwa dhambi ni mbaya na za mwizi ni 40.

    ReplyDelete
  5. yani ukisikia madudu ni TRA na TPA, yani huko kuna madudu yakutisha, Mhs bado wako wengi hao, wapige chini tu.

    ReplyDelete
  6. Hivi kwaLe tunapaswa kuitwa nchi maskini. Tukubali kuwa nchi ilikuwa haina viongozi. Na iligeuka shamba la bibi. Aliyepata nafasi anavuna hata wakumuuliza hayupo. Mafisadi hawa walitaka kutuvurugia aman yetu. Maana taifa moja Kuna watu wenye pesa zisizo ulizwa mbaya zaidi wanahonga malaya magari ya kifahari na nyumba. Watanzania tuseme ufisadi bac tuusapoti uwamu hii ya tano. Kwa kweli wania ya dhati ya kutukomboa kutoka kwa mafisadi . Mawaziri mliopita hamkuona hili. Mzee sita, nchemba, saada. Vp hapo. Aibu tutaua madudu mengi mwaka huu. Wafilisiwe Mali zao

    ReplyDelete
  7. Fyuuuuuuuuu
    Aende msoga kwa shemeji jake
    Huashi mtu mzima ovyo

    ReplyDelete
  8. Eeeh Mungu umetusikia waTZ,endelea kuonyesha madudu ya mabedui wasio hata na chembe ya huruma kwa taifa,msaidie na kumuongoza rais wetu na mawaziri wake kufanya kazi kwa ufasaha,wewe ukiwa ndio nguzo yao kuwaepusha na maovu yoteyote watenda mabaya wanayowawazia juu yao.nk.AMINA.

    ReplyDelete
  9. Hakuna cha kujificha awamu hii,MUTATEGULIWA TU NA MBINU ZETU CHAFU,shwaini zenu.

    ReplyDelete
  10. Thank you Jesus ,Tanzania was like a geto,any one could do any thing he/she want, for now I can think to do bussiness ,from here to my home land.

    ReplyDelete
  11. Hata wakifukuzwa kazi, LAZIMA WARUDISHE PESA ZOTE WALIZOIBA, YAANI WAFILISIWE........, haiwezekani waachwe wakazitumie, WAFILISIWE ...........HAPA KAZI TU.......

    ReplyDelete
  12. Uwiiiiiiiiiiiiiiiii,kumbe ndio maana Kagame alisema angekuwa na bandari umaskini kwenye nchi yake ingekuwa ndoto.AIBU KUBWA TANZANIA KWA KUHITAJI MISAADA TOKA NJE WAKATI TUNA UWEZO WA KUTOSHA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  13. Duh! Kwa kasi na mwendo huu, 'KALUME-KENGE' ATAKWENDA SHULE TU, maana moto umeshaanza kuichoma FIMBO, je FIMBO itakubali...???

    ReplyDelete
  14. Duuh,jamaa wanapiga pesa ndefu sana hawa, enzi za mwalimu Nyerere nasikia walikuwa wanaitwa wahujumu uchumi,ukionwa una maisha mazuri ghaflaghafla utachunguzwa na hatimae unakamatwa na polisi ueleze umepata wapi pesa,natamani TZ mpya iwe hivyo.

    ReplyDelete
  15. Akamate hadi mawaziri fisadi

    ReplyDelete
  16. HAO JAMAA NI WEZI SANA TENA WANASHIRIKIANA VITENGO VYOTE.

    ReplyDelete
  17. siku nyingine mkuu ingia idara ya viwango huko tena ndio usiseme

    ReplyDelete
  18. Tembelea wizara ha ardhi na DAWASCO mkuu. Hasa DAWASCO ya tegeta. Inanuka kwa madudu. Na wizara ya ardhi imezidi kunyanyasa watu. Hapa kazi tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad