Bunge Laanza kwa Spidi: Nape Apigwa Dongo, Aambiwa Anasumbuliwa Na Utoto

Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza jana mjini Dodoma na moto ambao wengi waliutabiri huku harufu ya ushabiki wa vyama ikitawala.

Katika zoezi la kumtafuta Spika wa Bunge hilo lililotanguliwa na maswali na majibu kwa wagombea nane waliojitokeza, Mgombea Uspika kupitia Chadema, Goodluck ole Medeye alikwaruzana kimtazamo na mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye.

Swali la Nape lililokuwa kati ya maswali matatu aliyoulizwa Ole Medeye lilionekana kumuudhi mgombea huyo. Nape alimtaka Ole aeleze kama ameacha tabia ya ubaguzi kwa madai kuwa Godbless Lema aliwahi kumtuhumu kuwa ni mbaguzi.

Ingawa Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Andrew Chenge alikataa swali hilo lisijibiwe akieleza kuwa halikuwa swali, Ole Medeye alihitimisha kwa kumueleza Nape alichokuwa nacho moyoni ingawa hakumtaja jina.

Kuna mbunge hapa aliniuliza swali ambalo kwa lugha za kibunge tunaliita ni swali la kuudhi. Mbunge huyo nimemsamehe, sina chuki naye kwa sababu najua kinachomsumbua ni utoto tu, akikua ataacha,” alisema Ole Mideye.

Uchaguzi huo ulikamilika na kumuwezesha Job Ndugai kuwa spika wa Bunge hilo baada ya kupata asilimia 70 ya kura zote.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tumeondoa zee la kukoroma bungeni
    CCM matuletea wendazimu navichaa
    Hata bunge halijaanza

    ReplyDelete
  2. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.
    Walianza chadema kuuliza maswali ya kuudhi, wakawakuta CCM nao wapo 'ready'.........safari hii, KUTACHIMBIKA ni madongo kwa madongo mpaka mtu atapike nyongo hahahahahaha HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  3. bunge la upendeleo watoto wa vigogo wamejaa bungeni na wengine watapewa ubunge kwa viti 10 vya upeneleo,yaani huku duniani haki hakuna,Benki kuu wamejaa pia watoto wa vigogo duuu

    ReplyDelete
  4. VIONGOZI WA CHADEMA NI UROHO WA MADARAKA NI MAFASIDI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad