CCM Yafuta Ushindi wa Mtoto wa Dk Abdallah Kigoda

Kamati Kuu ya CCM imefuta matokeo ya kura za maoni katika Jimbo la Handeni, mkoani Tanga ambako Omar Abdallah Kigoda ambaye ni mtoto wa mbunge wa zamani, marehemu Abdallah Kigoda alikuwa ameshinda.

Akizungumza jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jana kuwa kutokana na kufutwa kwa matokeo hayo, uchaguzi wa kura maoni katika jimbo hilo unarudiwa leo.

Alifafanua kuwa wagombea 11 waliwania nafasi hiyo lakini wawili kati yao, Kigoda na Hamis Amad Mnondwa walipata kura zaidi kuwashinda wenzao.

Mkutano mkuu wa jimbo la Handeni, ulimchangua Omari Kigoda kwa kura 296 akiwashinda wenzake wawili Hamisi Mnondwa na Athumani Lukoya waliokuwa wamechujwa kutoka miongoni mwa wanachama 11 walioomba nafasi hiyo.

“Lakini matokeo yanaonyesha hakuna mshindi aliyepata kura za kuridhisha kuingia katika ushindani na vyama vingine, ndiyo maana Kamati Kuu imeamua urudiwe,” alisema bila kutaja idadi ya kura walizopata wagombea hao.

Mchakato huo wa kupata mgombea unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dk Abdallah Kigoda kilichotokea Oktoba 12, mwaka huu nchini India.

Nape alisema marudio hayo ya kura za maoni yatasimamiwa na makada watatu wa CCM, Dk Maua Daftari, Dk Emmanuel Nchimbi na Abdallah Bulembo.

Nape alisema Kamati Kuu inaendelea na kikao chake cha siku moja ambacho kina ajenda ambazo hakutaka kuzitaja. Kamati Kuu imefanya uamuzi huo huku kukiwa na sintofahamu juu ya chama hicho kuanza ‘utaratibu mpya’ wa kuwateua watoto wa vigogo wa chama hicho wanaofariki dunia wakiwa wabunge au wagombea, kuwania nafasi iliyoachwa na wazazi wao.

Mbali na Omary, Goodluck Mtinga, mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi) Celina Kombani naye amepitishwa na chama hicho kugombea ubunge katika jimbo la Ulanga.

Utaratibu kama huo ulitumika katika Jimbo la Kalenga mwaka 2014, CCM ilipomsimamisha Godfrey Mgimwa, mtoto wa marehemu Dk William Mgimwa, kugombea ubunge katika jimbo hilo lililokuwa likishikiliwa na baba yake.

Mwaka 2012, CCM pia ilimteua Sioyi Sumari kugombea ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki kuziba nafasi iliyoachwa na baba yake, marehemu Jeremiah Sumari.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe mwenyewe umeshinda kwa wizi wa kura
    Shame CCM tangu urais hadi udiwani
    Ngoja tusimamishe misaada yetu hasa nyie walala hoi mliyoichagua CCM
    Mjue sisi Nani tunalipa kodi zetu ulaya Na USA
    Bora tusaidie wakimbizi toka ulaya mashariki kuliko kusaidia Africa hasa Tanzania iliyojawa na wizi ufahari ubi shoo WA viongozi WA CCM

    ReplyDelete
  2. Utoowa lini au kuolewa lini Nape

    ReplyDelete
  3. Kama kawaida yenu CCM kupitisha watoto wangu kurithi uongozi WA mama zao au baba zao
    Mtaisoma

    ReplyDelete
  4. Chama Na serikali washageuza vya kurithishana kumamazao wasenge hao

    ReplyDelete
  5. hamjui km ccm wana itikadi za kifalme

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad