Chadema Kufungua Kesi Kupinga Agizo la Polisi Kuzuia Kuagwa Mwili wa Alphonce Mawazo.

Baada ya zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kushindikana kutokana na jeshi la polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku mikusanyiko ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa madai ya kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Mwanza, hatimaye viongozi wakuu wa kitaifa wa Chadema pamoja na familia ya marehemu wameamua kwenda mahakamani kesho kutafuta haki yao ya kisheria.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mwanza  na mwenyekiti wa Chadema taifa Mh. Freeman Mbowe akiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mh. Edward Lowassa.

Naye Mchungaji Charles Lugiko ambaye ni baba wa marehemu Alphone Mawazo amelaani  kitendo cha askari polisi kwenda hadi nyumbani kwake eneo la Nyegezi na kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa ajili ya kuuaga  mwili  wa  marehemu Mawazo.

Alphonce Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha katoro wilayani Geita.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahahahah!! Hizo hasa ndio kazi zenu WAPINZANI, kutafuta wapi pa kupinga mkapinge, kuongea na waandishi wa habari kila siku, kususia bunge n.k hahahahahaaaaa HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. Ipo siku UNYANYASAJI, UKATILI KWA WANYONGE WANAODAI HAKI ZAO NDANI YA SERIKALI HII KIPOFU NA KIZIWI itakuja kurealize kumbe UPINZANI WANAPOINT kwa wanachokifanya. Na kama Serikali iko sahihi kwanini inawazibia WAPINZANI kila wanapotaka kufanya jambo na wananchi? MPAKA KWENYE MSIBA SERIKALI INATAWANYA WAOMBOLEZAJI KISA NI UPINZANI WALIO WENGI WAMEKUSANYIKA KWA AJILI YA MWENZAO ALIYETANGULIA MBELE YA HAKI?!! Aibu gani hii Tanzania, halafu mnasema eti kisiwa cha amani...! Hata haya hamna?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad