CHADEMA Wamzawadia Mke wa Lowassa Ubunge wa Viti Maalumu..Mwenyewe Aibuka na Kutoa Maamuzi Magumu na Kusema Haya

Mke wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, Regina Lowassa, ameikataa nafasi ya ubunge wa viti maalum aliyopewa na kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani.

Kwa mujibu taarifa wa kutoka familia ya Lowassa iliyotufikia, Regina anaichukulia kwa heshima kubwa nafasi hiyo, lakini anaamini ataweza kushughulikia matatizo ya akina mama na watoto akiwa nje ya bunge.

"Naishukuru kamati Kuu ya chama changu kwa heshima hii kubwa waliyonipa na ninaithamini sana, lakini naamini nitaendeleza mapambano ya kuwaletea akina mama mabadiliko kwa ufanisi zaidi nikiwa nje ya bunge," amesisitiza mke huyo wa waziri mkuu wa zamani katika taarifa hiyo.

Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi wa kumpa Regina nafasi ubunge viti maalum kutokana na mchango mkubwa aliyoutoa wakati wa kampeni ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia upatikanaji wa majimbo mengi tofauti na uchaguzi wa mwaka 2010.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie Chadema kweli mnamsanifu Regina alitegemea na kumuahidi ufirst lady lazima ataupta kwani mmejipanga CCM haioni ndani mmelamba turufu Mr. Edo mhhh anahaki ya kukataa ofa yenu ufirst lady na ubunge wapi na wapi

    ReplyDelete
  2. Regina Yule CCM damu ataweka wapi sura yake mbele ya CCM basi tu Chadema hawajajitambua ndo maana hawatakuwa na ubavu wa kuishinda CCM wanakurupuka ovyo ovyo mambo yao ya kihuni huni

    ReplyDelete
  3. Pendekezo langu
    yeye awe chachu za ukawa popote

    ReplyDelete
  4. Regina na Edo ni CCM Damuuuu,,,, ukawa mtasubiri sanaaaa

    ReplyDelete
  5. LAKINI UKAWA KWELI NI TUNDU CHAFU HATA LIKIPAKWA PERFUME BADO LINANUKA TU ,,,, TANGU LINI LOWASA NA MKEWE WAKAWA CHADEMA ?YAANI MMECHEZEWA PICHA KAMA WAPUMBAFU MSIOKUWA NA AKILI ... WOTE MNAJUA LOWASSA NI CCM DAMU HATA IWE VIPI HAIWEZI MTOKA HALAFU NYIE MWAMUONA MWANA MAPINDUZI. , HAYA KAZI KWENU NA CHAMA CHENU SASA NDIO KWISHINEHI,,, MAGUFULI NDIO ANABADILISHA NCHI SASA NA MIAKA MINGINE 5 ATAPIATA BILA MPINZANI NA AKITAKA ATAENDELEA KAMA MUGABE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio tunakoenda,akimaliza miaka mitano kwa staili hii aliyoanza nayo,na TZ ikabadilika atapita kwa miaka 5 mingine na akimaliza tutaweka mabango aendelee maana watu wa namna hii Tanzania wachache.katiba sio misaafu,tutavunja tu hilo likatiba lao.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad