DIAMOND Kuna Ulazima Gani Kuishi na Mama Yako Katika Umri Huo? Sio Kosa ila Kuna Ulazima wa Kujitenga..


KWAKO mkali wao katika anga la Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Mambo vipi mzazi jembe? Hongera sana kwa ushindi mnono ulioupata hivi karibuni katika Tuzo za MTV EMA 2015 jijini Milan Italy, umezidi kuliletea taifa letu heshima.

Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima. Namshukuru Mungu naendelea kupambana na kazi zangu kama kawaida ili mkono uende kinywani.Nimekukumbuka leo kwa barua kwani kuna jambo nataka nikushauri. Ikiwezekana ulichukulie hatua fasta na nina amini heshima yako itazidi kuongezeka hususan katika eneo la uhusiano na baadaye ndoa.

Natambua jinsi gani unampenda mama yako. Najua mama kwako ndiyo kila kitu na ndiyo maana unatamani kukaa naye karibu. Unatamani wakati mwingine hata usiende kufanya shoo ili uwe karibu naye, lakini unashindwa tu pale unapobanwa na majukumu ya kimuziki.

Muziki unakutenganisha na mama kwa sababu ni kazi lakini vinginevyo, ungekuwa mtu wa kushinda naye nyumbani. Pamoja na mapenzi hayo kwa mama yako mzazi, hadhi uliyonayo sasa hivi kama msanii mkubwa au namba moja Bongo, sioni kama kuna sababu ya kuendelea kukaa nyumba moja na mama, japo una nia njema kufanya hivyo.

Familia zetu za kiswahili tunajuana, sisemi kwamba ukikaa na mama huku ukiwa na mpenzi wako au mkeo ni makosa, lakini mimi naona ni busara zaidi ukawa mbali na mama yako. Ikiwezekana kama hiyo nyumba mnayoishi umemjengea yeye, basi ni bora wewe ukakae sehemu nyingine ili uwe huru zaidi.

Tumeshuhudia hivi karibuni kuondoka kwa mpenzi wako, Zarinah Hassan ambaye amerudi kwake nchini Afrika Kusini. Nyuma yake kulikuwa na maneno ya hapa na pale. Ikasemekana kuna mambo yalikuwa hayaendi sawa, ‘figisufigisu’ za mawifi sambamba na mama’ko zilikuwa zikitokea.

Hayo manenomaneno yasingeweza kutokea kama ungekuwa unakaa mbali naye. Umemjengea mama nyumba nzuri lakini si lazima mkae pamoja. Wewe waweza hata kupanga, mama yako akabaki hapo akainjoi maisha.
Wewe unahitaji kuwa na mji wako. Uwe na familia yako ambayo inajitegemea, hivyo ni busara zaidi ukajitenga na mama, si kwa nia mbaya lakini yeye inapendeza zaidi kama utakuwa unakwenda kumsalimia tu kadiri uwezavyo na hata yeye kuja kwako kukusalimia pale anapojisikia.

Faragha yako na mkeo ni nzuri ikaheshimika. Mjiachie wenyewe na watoto wenu mtakaojaliwa. Inapendeza watoto nao wakifunga safari kwenda kumsalimia bibi yao. Hayo ndiyo maisha mazuri, tena yenye hadhi yako kama staa namba moja Bongo.

Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa mzazi na nikusihi ulifanyie kazi suala hilo maana linaleta heshima kwako na linasaidia kuondoa migogoro ya hapa na pale ambayo naamini kabisa inaepukika.
Nikutakie maisha marefu yenye baraka na uendelee kutupa burudani kwani umezaliwa kutuburudisha!
Ni mimi nduguyo,

By Erick Evarist/GPL

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siyo mama yake pekee mpaka dada yake wanaingilia maisha yake ya mapenzi wakati ya kwao ni aibu zaidi!

    ReplyDelete
  2. Barua nzuri sana na inaushauri mzuri sana! Nikutakie mafanikio mema.Diamond fanyia kazi hayo mapendekezo

    ReplyDelete
  3. Kweli kabisa, umempa ushauri mzuri sana naakiufanyia kazi ataona matunda yake yaliyo bora.

    ReplyDelete
  4. BORA ZARI AMERUDI KWA AIVAN MAISHA YA KIZUNGU ZAIDI, SIO KWA DAI UKOO WOTE UMEJAZANA NYUMBA MOJA... ULIMBUKENI MTUPU... KISA CHA KUPATA UGONJWA WA MOYO!!!!

    ReplyDelete
  5. yaani mdau umeongea kitu cha busara sana. Dai anatakiwa akae yeye na mkeo na sio ukoo mzima, kuingilia mapenzi ya Dai. I know she's good mother but kunamipaka mtoto akisha kuwa na family yake. Dai you need your daughter close to you.

    ReplyDelete
  6. Umeongea point sana, na nafuraha watanzania Wengi sasa wameliona hili maana mwanzo wa sekeseke tulijitokeza kusema hata kwenye page ya mama ake IG na ya esma lkn watu baadhi waliona kama hatuwatakii mema. Na walidiriki kusema eti wanakula matunda ya ndugu yao mhhh maajabu haya hivi kila mzazi akisema aende kwa mwanae eti kisa alimsomesha au kumlea kwa shida hivi mjini kutatoshaa??? Kuna watu Wengi waliwalea watoto wao kwa shida mbona hatujawahi kusikia wanataka kuja kuishi kwenye majumba mazuri ya watoto wao? Diamond asipoangalia hatakaa afurahie maisha ya mahusiano kwa mtindo huu. Ataishia tu kubadili wanawake maana hakuna mwanamke atakae kubali kuishi nyumba moja na mama mkwe, mawifi, na mjomba juu kwenye nyumba moja. Ajue watu wote tunawapenda wazazi wetu sio yy tu. Huu upendo wake haujengi

    ReplyDelete
  7. ampangishie mama yake yeye akae na familia yake sio mkewe kukaa na wifi na mama mkwe midomo lazima itokee tuu na mke kukwazika

    ReplyDelete
  8. that's right, probably Zari doesn't want deal with uswahili anymore lol

    ReplyDelete
  9. Mama ndo fundi bibi

    ReplyDelete
  10. DIAMOND WW NI MALAYA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad