BAADA ya muigizaji nyota Wema Sepetu ‘kumtusi’ mpenziwe wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa kudhihaki zawadi ya bei chee ya gari aliyowahi kumnunulia, rais huyo wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), juzikati aliibuka na kumjibu kuwa amefanya mambo ya ‘Kiswahili’.
Akizungumza ofisini kwake Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Diamond alisema katika maisha kila mmoja ana ndoto zake, hivyo ni jambo jema kwamba amefanikisha, lakini hata hivyo, akasema hatua aliyofikia yeye siyo ya kufanya mashindano na mtu, badala yake ni kuchapa kazi kusaka mafanikio zaidi ya maisha yake.
“Kiukweli kabisa nampongeza Wema kwa kununua gari maana hiyo ndiyo ilikuwa mipango ya maisha yake, maneno anayosema kwamba mimi nilimnunulia gari la elfu thelathini ndipo nilipomuona wa ajabu. Sikuona umuhimu wa kunizungumzia pale.
“Hayo ndiyo mambo ya Kiswahili. Mimi siyo mtu wa kushindana kununua gari tena, maana hatua hiyo tayari nimeshapita, zaidi nawaza kupiga kazi na kujitengenezea maisha yangu mapya yatakayoweza kuifanya familia yangu iishi kwa raha na amani kipindi chote cha uhai wangu, najua kuna watu bado wanafikiria mimi ni limbukeni wa vitu kama zamani, kwa sasa sifikirii mashindano, ninaangalia kazi zinazoweza kuniingizia kipato tu,” alisema Diamond.
Katika pati aliyoiandaa hivi karibuni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Wema pamoja na mambo mengine, aliwaonyesha waalikwa zawadi ya gari aina ya Range Rover aliyojinunulia, akitoa maneno yaliyoonyesha kumponda Diamond, kwamba ameinunua kwa kiasi cha dola za Marekani 90,000 (karibu shilingi milioni 200 za Kitanzania), tofauti na watu wanaojikweza kwa ‘vigari vyao vya elfu thelathini’.
Source:GPL
Pumbavu wote hawa
ReplyDeleteHayo mambo Ya kizamani kabisa mtu ashindanie maisha yake sio gari 💪🏿😷
DeleteDomo anasahau anapompigia madongo Wema, hukaa kimya, sasa yeye kaona issie.
ReplyDeletekwanza Dai hakutoa milion 30, Wema aliiuza gari yake ndogo na Dai akamuongezea.
ReplyDeletekumbe Wema akisema kitu Dai kiamuuma hee! anasahau anavyomtoe maneno ya chombo!
ReplyDeletehana lolote aseme ukweli kama kaumia Wema kamuonyesha anaweza, kakonda ghafla
ReplyDeleteatakosaje kukonda anaoa wazee kila uchao mara huyu mara yule, angaza inamuhusu.
Deletekunya anye kuku, akinya bata kaharisha! Domo alifikiri kuwa na bi kizee kutamfanya Wema apagawe, kumbe kaonyeshwa kitu hawezi kua ford.
ReplyDeleteDiamond kawa mdogoooooo kama pilton. kabakia kuonyesha picha la mimba hahaaa,
ReplyDeletemafumbo na maneno ya uswazi kwa Wema kayasahu, leo kaona gari limemshuka na ajuza wake,
ReplyDeleteGari gani mtumba huo
DeleteFyuuuuuuuuuuu
kaishiwa na kiki Domo kabakia kumpongeza kiaina Wema. alifikiri kuzaa kutamfanya aonekane bingwa kumbe migogoro kibao state house ya kwamtogole.
ReplyDeleteDai imemuuma sana aseme ukweli, alijiona yeye ndo staa, kasahu kamkuta Madam anawaka kitaambo.
ReplyDeleteMTENDA AKITENDWA HUJIHISI KAONEWA. KAA KIMYA DOMO
ReplyDeletekwa umri mliofikia mnatakiwa kujielewa na kujitambua na si kushindania magari na kuweka mambo yenu hadharani mtandaoni,mmekua sasa.....!ala...
ReplyDeleteKuna watu wanamiliki magari mengi na wanayatumia kufatana na rangi za nguo wanazovaa, Najuwa umenunua gari sababu tu yakutowa majibu kwa Chubu, HASIRA-HASARA watanzania wanawategemea nyie nyote ktk kupepea bendera yao, $90,000 (2000-ML) kwa nini usifunguwe kampuni usaidie ajira kwa wa-TZ? wewe una gari zingie nzuri tuu mbona zina tosha kabisaa kwa maisha ya hapa bongo?? ama kwanini usiwasaidie ndugu zako huko kwenu kijijini maana lazima wana matatizo mengi tuu!! akili yako imekutuma vibaya ukaona umjibu mwenzio kwa kununua Gari la pesa nyingi hata kama nduguzo wanashida!!!!?? ANGALIZO: watanzania wanakutazama kwa macho yao yote na wanaku tathmini una biashara gani unafanya, *CHIBU angalia usipandwe midadi kwa majibu hayo ya Range Rover waaala si lolote we mwananume, usiharibu mipango yako eti na wewe ukaamua kununua ndege, kumbuka wanawake walio wengi wanapewa tuu hawatafuti, kaza buti endelea kuwasaidia wasanii chipukizi, watu wote wanajua kama we uwezo unao, umesha piga hatua nzuri tuu achana na maneno, Na nivizuri unajitambua kama level hiyo ya viji-magari ulishapita!! big-up and give-up songesha
ReplyDeleteHajuwi haya moviies zake tutakopi na kuuza bei ya sh 100
DeleteKu
Hakuna kujielewa wala nini Domo kaumiaaa Mara matapishi Makombo Hajanizalia Simtaki uswaziiii kuuutwa kudhalilisha Wanawake
ReplyDeleteKumbukeni aliumia toka Benzi asiumie leo Range 2015 tena from her to her!!!
Kwa shobo la 40ya princess tulitegemea bonge la zawad kwa bby mama lkn wapiii anajijua kama wako kwa mkataba tu wasiharbu udhamini lkn yy si bby father
Mr. Matapishi Na Kajala pia?
Hata mchambeje domo mkali
DeleteSasa atanunua helkopta tuone huyo Wema atanunua
Anaishi nyumbani ya kupanga hakiendani kesho
ilo nalo neno mdau Anony 7,21 PM dharau zoote na maneo ya shobo kwa Wema leo kajibiwa moja tuu kakonda ghafla.
ReplyDeleteMnaosema Diamond Ana mtoto nani???ujanja wake wote mbona kashindwa kuthibitisha DNA ya mtoto wa Zari ogopa waganda wewe. Watanzania acheni kishabikia msivyokuwa na uhakika navyo
ReplyDeleteMimi Nina asilimia 100 Yule mtoto zari kampa Nasib ili apate ummatufu,Yule mtoto kazaa na mume Wa mtu bonge ya tajiri anaishi dar anaitwa katunzi mzamil
ReplyDeleteWatu wanacomment tu kama hawana vichwa. Daimond atabaki kuwa Daimond na hata Wema hawezi kumfikia. Juhudi zake mwenyewe ndio zimemfikisha hapo alipo. Awe na kibibi au jimama haiwahusu. ujinga tu na ulimbukeni wa kujisifia magari. watu wanasifia familia wewe unasifia magari. Halafu bora ya zari aliyempa mtoto. wewe unayesema mtoto wa tajiri, huyo tajiri yy hataki mtoto mpaka amwachie Diamond, acheni wivu wenu usiyo na maana. Wema ana wivu na anatamani Diamond amrudie ndio maana anafanya vitu akidhani anaamuumiza roho Diamond kumbe anajiumiza yeye. Yeye ambaki na Luis na Diamond abaki na Zari wake. Wengine tuache umbea na uchonganishi kujifanya tunajua maisha ya watu wakati ya kwenu yanawashinda.
ReplyDelete