Dodoma: Rais kuhutubia Bunge na Waziri Mkuu kujulikana kesho, UKAWA bado hawasomeki

Rais wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli, amewasili jana hapa Dodoma tayari kwa kulihutubia na kulizindua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Magufuli, katika hotuba yake, anatazamiwa kugusia mwelekeo wa Serikali yake ya awamu ya tano na nini kinalengwa kufanyika. Rais Magufuli anatazamiwa kukumbushia utekelezwaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015 na kutaja vipaumbele vya Ilani ya CCM ya 2015-2020 na jinsi vitakavyotekelezwa.

Hadi sasa, Wabunge wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vya CHADEMA,CUF na NCCR-Mageuzi wameshawasili kwa wingi hapa Dodoma na hata jana wote waliopo hapa Dodoma walishiriki kupiga kura za kumchagua Spika wa Bunge: Job Yustino Ndugai. Ikumbukwe kuwa jana, kura zote za Wabunge ziligawanywa kwa wagombea wa CCM na CHADEMA tu kwakuwa wagombea wengine sita hawakupata kura.

UKAWA wanasemwa kuwa wamejipanga kugomea hotuba ya Rais Magufuli kwa ima kutoingia Bungeni wakati wa hotuba hiyo au kuingia na kupiga kelele. Lakini, taarifa za kiintelijensia katika viunga vya Dodoma hazijathibitisha yasemwayo. UKAWA bado hawasomeki. Wanaendelea na vikao vyao vya siri kwa umakini mkubwa huku wakiwa wamoja kuliko muda wowote tangu UKAWA uundwe. UKAWA na CCM wataanza mtanange wao wa hoja za haja hivi karibuni Bungeni Dodoma.

Kila kitu kipo tayari. Kila mtu yupo tayari. Kila chombo cha habari kipo tayari. Wananchi wako standby. Kumsikiliza Rais, kushuhudia Waziri Mkuu mpya, Naibu Spika mpya na mnyukano usio na mfano katika kuendesha Taifa letu kidemokrasia. Hapa CCM, pale UKAWA. Hapatoshi Dodoma!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe unayefyatuka kwa kusema "sisi wananchi tumewatuma dodoma......"ni mpuuzi mnafiki wa ccm,tena ni mbunge mteule wa ccm.unajua UKAWA ni wabunge waliochaguliwa na wananchi na wabunge WENGI wa CCM ni wabunge figisu-figisu waliopachikwa pale na Tume ya taifa ya uchaguzi.hiki ndicho kipaumbele kinachopaswa kuwekwa wazi,kuheshimiwa na kufanyiwa kazi[siyo ndogo] na wabunge hawa wa wananchi.Dodoma itaelewa,Tanzania itaelewa na Ulimwengu mzima utapaswa kuelewa.Haya ni mapambano endelevu ya kidemokrasia na kisiasa kwa UHAI WOTE WA MIAKA MITANO WA BUNGE HILI LA 11 LA JAMHURI.UKAWA iliibiwa ushindi mezani na UKAWA haitorudi nyuma kuuelezea ukweli kwa umma wa watanzania.sasa hivi POLISI ikitumiwa kikamilifu na CCM wamekwishapiga marufuku mikutano ya kisiasa[acha hii ya kupata wabunge majimbo yapatayo matano ambayo bahati mbaya uchaguzi haukufanyika] kujenga demokrasia,wanachama hawaruhusiwi kukutana na ulinzi wa polisi unaweza kuueleza vizuri wewe unayewaona mitaani.TUMAINI LA SAUTI YA WANANCHI LIMEBAKI NI BUNGE PEKEE,IKISHINDIKANA BASI MHESHIMIWA MAGUFULI KWA UWEZO ALIOPEWA NA KATIBA YA NCHI ITALAZIMIKA ALIVUNJE NA KUTANGAZA TAREHE MPYA YA UCHAGUZI MKUU.RAI,TUSIFIKE HUKO TUWAHESHIMU WABUNGE WETU BILA HILA YA KUJARIBU KUIKOMOA UKAWA,HAIKOMOLEKI.

    ReplyDelete
  2. HIZO NI SIASA TU, YETU MACHO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad