Dr.Tulia: Nina Sifa Zote Za Kuwa Mbunge.....Sijapandikizwa ili Niibebe Serikali

Mgombea unaibu spika kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Tulia Ackson Mwansasu, amekanusha madai kwamba amepewa nafasi hiyo kama pandikizi ili aibebe Serikali.

Amesema madai kuwa ataibeba Serikali kwa kuwa ni mbunge wa kuteuliwa hayana msingi kwa kuwa haendi bungeni kumtumikia rais bali kuwatumikia Watanzania.

Rais John Magufuli Jumatatu wiki hii alimteua Dk. Ackson kuwa mbunge wa kuteuliwa na kutengua nafasi yake ya naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali aliyoteuliwa hivi karibuni na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Ni kweli nimeteuliwa na rais, lakini nakwenda kufanya kazi za Watanzania, nikipata nafasi ya kuwa naibu Spika madai kuwa nitaibeba serikali hayapo kwa kuwa nitafanya kazi za Bunge ambazo ni kuisimamia, kuishauri na kuiwajibisha serikali,” alisema Dk. Ackson ambaye juzi usiku alipitishwa kwa kauli moja na wabunge wa CCM kuwa mgombea wake wa unaibu spika.

Alisema ni vyema wabunge wakawa na imani naye na kumpa ushirikiano wa dhati ili atekeleze majukumu yake ipasavyo.
Katika hatua nyingine, vita ya unaibu Spika wa Bunge la 11, imemalizika, baada ya, Dk. Ackson, kupitishwa kwa kauli moja na wabunge wa CCM kugombea nafasi hiyo.

Awali kulikuwa na mvutano wa ndani kwa ndani baina ya wabunge wa chama hicho, ambao waligawanyika kwa baadhi kumtaka Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwenda wewe ulivyonda haraka haraka hivi
    Sisi si wajinga hivyo
    Haijatoke Tanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. UTAUMWA SANA, HAKUNA WA KUKUTIBU!!!
      NDO'BASI TENA
      ALOPEWA'KAPEWA

      Delete
  2. Naibu mwanasheria mkuu
    Kwa ajiliM 200
    Mara ugombee uspika CCM wakachemsha kwani ulitakiwa uaache unaibu mwanasheria
    Mara unajitoa unagombea unaibu spika
    Hiiii inashangaza hata kwa maiti
    Tena una PhD ya sheria
    Shame you CCM
    Utapita kwa wingi WA wana CCM lakini ni mkono wa Mtu
    Utawakuta bungeni wenye sheria Kama yako wanavyoijua sheria Na kanuni za bunge

    ReplyDelete
    Replies
    1. Imewauma hiyoooo........imewachoooooma kama pasi..... CCM woyeeeeee!!
      Mtakondaje mwaka huu.........MTAISOMA NAMBA

      Delete
    2. Mtaisoma namba nyiye muishio bongo
      Ughaibuni tuna raha zetu

      Delete
    3. Kama unaona kuwa ugaibuni ndio umefanikiwa kwa nini unahangaika na habari za Tanzania? wewe wala haujielewi, na huko unafanya kazi za kitumwa na utakuwa mtumwa mpaka mwisho maana haujitambui

      Delete
    4. Lakini hatuibi na mafisadi
      Tumechoka kusaidia ndugu zetu kwa ajili ya CCM

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad