Edward Lowassa wa Ukawa Ajitokeza na Kumkosoa Dr John Magufuli, Amuhoji Maswali Matatu

Aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.
“Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi,” alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.
Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.
“Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao,” alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo. Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.
Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.
Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.

Post a Comment

26 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. LOWASA UNACHO KITAFUTA HAKIJULIKAN KILA KUKICHA UNA SABABU ZISIZO KUWA NA MSINGI KWANINI USIRUDONJWA HUWEZI IKWENU UKAGUZIACHUNGE NQ'MBE KAMA ULIVYO SEMA AWALI UKISHINDWA UCHAGUZI SASA BADO UNAKALIA MAMBO YA SIASA WW MWENYEWE NI MGONJWA KUNA WAKATI UNAJINYEA ITAKUWA AJE WATAKA KUWA RAIS WW NI FASIDI NUMBER MOJA

    ReplyDelete
    Replies
    1. hivi wewe ulizaliwa upande gani?

      Delete
  2. Muheshimiwa nakumbuka kabla ya kutangaza nia ukiwa CCM ulichangia sana mashuleni,misikitini na makanisani,sio mbaya na wewe kwa namna unavyoweza ukaendelea kusaidia kama kweli unajali wananchi wa TZ.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. utakufa masikini wa akili..

      Delete
  3. MMH,UKOSOAJI HUU UNGEUNZA WAKATI UKIWA WAZIRI MKUU WATANZANIA TUNGEKUWA MBALI SANA,LOL!

    ReplyDelete
    Replies
    1. nilikuwa nashangaa kwanini watanzania ni masikini? ila sasa nimegundua kuwa sababu kubwa ni watanzania wengi kwanza ni masikini wa akili kama wewe mtoa hii comment..

      Delete
  4. ULITUPA SERA HIZI NA WATANZANIA TULISIKIA LAKINI HATUKUZIPENDA MAANA TUNA AKILI YA KUJUA KWELI NA UONGO, TUMEMCHAGUA AMBAE SERA ZAKE TUNAAMINI ZINAWEZEKANA, HATA WEWE USINGEMALIZA MATATIZO YA WATANZANIA KWA SIKU 3 TU IKULU, NI MCHAKATO! ULIKUWA WAZIRI MKUU KWA MIAKA MINGAPI VILE? NA WAZIRI MIAKA MINGAPI VILE? MBUNGE WA MONDULI MIAKA MINGAPI VILE? TUMERIDHIKA NA MAGUFULI WETU TUACHIE WENYEWE, ADAA HII HAIUSU WATO, WAJUKUU WALA VILEMBWE WAKO MAANA HAWASOMI SHULE HIZI, PUMZIKA UBORESHE AFYA YAKO ILI TUMHUKUMU MAGUFULI MWAKA 2020 NA KAMA HATUTOONA KAZI TU TUTAFIKIRIA TENA KUKUPA WEWE AU MWINGINE AJE

    ReplyDelete
  5. ULITUPA SERA HIZI NA WATANZANIA TULISIKIA LAKINI HATUKUZIPENDA MAANA TUNA AKILI YA KUJUA KWELI NA UONGO, TUMEMCHAGUA AMBAE SERA ZAKE TUNAAMINI ZINAWEZEKANA, HATA WEWE USINGEMALIZA MATATIZO YA WATANZANIA KWA SIKU 3 TU IKULU, NI MCHAKATO! ULIKUWA WAZIRI MKUU KWA MIAKA MINGAPI VILE? NA WAZIRI MIAKA MINGAPI VILE? MBUNGE WA MONDULI MIAKA MINGAPI VILE? TUMERIDHIKA NA MAGUFULI WETU TUACHIE WENYEWE, ADAA HII HAIUSU WATO, WAJUKUU WALA VILEMBWE WAKO MAANA HAWASOMI SHULE HIZI, PUMZIKA UBORESHE AFYA YAKO ILI TUMHUKUMU MAGUFULI MWAKA 2020 NA KAMA HATUTOONA KAZI TU TUTAFIKIRIA TENA KUKUPA WEWE AU MWINGINE AJE

    ReplyDelete
  6. Mpuuzeni huyo na mawazo yake ya kibangi, Hivi leo angekuwa raisi pesa angetoa wapi ya kuwasomesha hao wote bure?? Labda ukawa wangesafirisha madawa ya kulevya tani 3 Afrika ya Kusini si ndiyo biashara zetu!!!

    ReplyDelete
  7. Maskini! kuweweseka hakuishi tu?,sasa unamuuliza maswali Magufuli akiwa kama nani kwako,maana umesema hutambui matokeo na kwamba wewe ndio mshindi.Ni wa kuombewa huyu mzee jamani.

    ReplyDelete
  8. Maelekezo ya mh Raisi JPM mbona yako wazi tu! tena kiswahili chepesi kabisa kwamba kuanzia Januari 2016 wanafunzi hawatalipa ada sasa unauliza waliopo shuleni je? khaaaaa ! sasa huelewi nini hapo rAhIsI wa Ukiwa? wanafunzi ni wale watakaokuwepo shuleni.mwaka 2016. Hebu nenda Ujerumani kwanza ukapotezee kidogo. mawazo na uta

    ReplyDelete
  9. Kweli TZ ina wajinga wengi mno

    ReplyDelete
  10. Lowasa unahamuuuuu,,,,

    ReplyDelete
  11. Eti 'Lowasa wa ukawa ajitokeza kumkosoa Dr. John Magufuli' bila haya wala aibu!! Wao wameshasema kwamba hawamtambui, sasa anamkosoa kama nani?? mfyuuuuuu. AMUWACHE AFANYE YAKE, YEYE HAYAMUHUSU...........HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  12. Hayo maswali matatu akamuhoji yule alo-badilisha gia angani, na kusababisha 'dege' likaporomoka kwa spidi ya 120.......

    ReplyDelete
  13. EDWARD LOWASA? NDIO NANI....??

    ReplyDelete
  14. Watanzania wakisema YES, nani wa kupinga?

    ReplyDelete
  15. prezida wa ukawa we waache watanganyika wamezoea umasikini, kujifungulia chini, kufa kwa kukosa dawa, elimu duni n.k. waache baba wa moja havai mbili.

    ReplyDelete
  16. lowasa ni mjinga kwa kifupi

    ReplyDelete
  17. Tanzania ni yetu sote sio yenu pekee yenu, mawazo yenu ni sahihi kwenu lkn sisi tulio wengi tumemchagua Dr JPM, Na demekrasia inawapa haki walio wengi, mikoa 4 kwa 26 bado mnasema? majimbo 190 kwa 60 hamuelewi? kubalini matokeo mjipange 2020 ndio uungwana, fanyeni kazi maana sasa NI KAZI TU, MANENO KINONDONI!

    ReplyDelete
  18. SIJAKUELEWA WEWE ENOUNOMOUS WA 10:05 PM KWA HIYO LOWASA NI WA ELIMU YA SASA?

    ReplyDelete
  19. Jamani nyie na rais wenu Lowasa ndiyo mnaongoza kwa kukwepa kodi na ndiyo maana k/koo wote walibadilika na ku-support Ukawa hasa Chadema kwa sababu kubwa ya mashine za mlipa kodi, ni mtu gani atamchagua rais asiyesema atapambanaje na rushwa, ufisadi, ukabila, ukanda na udini? haya yote ni tatizo kwa nchi yetu. Ni nani atamchagua rais amabaye hasemi atakusanya kodi vipi amabayo serikali zote duniani zinaendeshwa kwa kodi.Nani atamchagua rais asiyeweza hata kujieleza hata kwa dakika kumi? Nyie ndiyo watu wa ajabu ambao mlisema elimu itakuwa bure kwa kuweka rehani gas na madini mengine ya nchi yetu. Niwaulize nani anaweza kumuweka rehani mke, mume au mchumba wake ilifanikishe mambo yake? nyie ni mayawani na ndiyo maana mwishoni ikaonekana anayefaa kuliongoza taifa hili ni Dr Maghufuli tu. Hat mz Slaa aliwauliza akina Mzee Mbowe kuwa Lowasa ni Asset au Liability? waulize walivyomjibu Dr Slaa na kilichotokea ndiyo hicho kikichangiwa na kulitangazia taifa kuwa serikali ya Ukawa itakuwa rafiki wa Mama Ntilie,BodaBoda na Machinga halafu itakuwaje? hao bodaboda ndiyo vinara wa uhalifu hapa mjini na mikoani. Kwa maana srikali ya UKAWA ingekuwa karibu na wezi, majambazi, wanga na wachora ramani kwa ajili ya kufanikisha uhalifu. Uwzi kupata urais kwa njia hiyo labda kama nchi haina mwenyewe, nwashauri Ukawa waende na mgombea wao wakagombee SOMALIA au IRAQ wanaweza kufanikiwa.

    ReplyDelete
  20. unacho kisema wewe hukielewi ndo mana mnatukana matusi

    ReplyDelete
  21. Nyie ndiyo hayawani kwa kuwaleta ma -strategist toka kwenu Kenya na mmeshindwa. Ili kuonyesha kuwa uraia wenu una mashaka wamekamatwa na wataendelea kukamatwa ili wananchi wajue kuwa nyie ni WAZANDIKI wa taifa hili na laiti mngefanikiwa uenda sasa nchi hii ingebakia mifupa halafu nyie mnasepa mnaenda kwenye nchi yenu ya ahadi. Wewe ndiyo ujui ila kila kitu kina fahamika na haitatokea nyie kupewa ridhaa ya kuongoza taifa hili kwa nia yenu ni mbaya kwa sababu hili siyo taifa lenu mnasema mna nchi yenu ya ahadi aaambapo pia hamtafika mtaishia njiani.ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad