Edward Lowassa/Zitto Kabwe Wapeleka Kilio CCM

Hawa jamaa wawili kwa kweli kwa pamoja tunaweza kusema wamepeleka kiliomtaa wa Lumumba, waswahili husema kwa mjinga huenda kicheko lakini kwa mwelevu huenda kilio.

Ujio wa Lowassa UKAWA umepeleka kilio kikubwa sana CCM japo kuwa wanajikazakinyasa wanakufa na Tai shingoni. Majuzi Mh. January Makamba aliita waandishi wa habari na kujinasibu eti CCMimepata wabunge 176 mpaka sasa na kufanikiwa kugomboa majimbo 11 yaliyokuwa yawapinzani.

Sasa habu ona hapo chini kilio Lowassa alichokipeleka CCM ambacho Makamba hakupenda kutaja.

1. Viti maalumu vya CCM vimepungua kwa 40% toka 79bunge lilopita la10 mpaka 62 bunge la11. Wakati CHADEMA na CUF viti hivyo vimeongezeka haya ni maumivu makubwa

2. CCM imenyang`anywauongozi wa majiji 4 kati ya majiji 5imebakiwa na uongozi katika jiji moja tu la Mwanza,. Majiji yafuatayo CCM nichama cha upinzani , Jiji la Mbeya, Jiji kuu la Dar-es-Salaam, Jiji la kitaliila Arusha na jiji la Tanga ambalo ilikuwa ni ngome yao, ngome imevunjwa.

3. Ruzuku ya CCM imepungua kwa 40% kutokana na kuraza rais alizopata , mgao wa ruzuku utakuwa 60 kwa 40 kwa maana 58% alizopataRais Magufuri kwa desilimali ya karibu itakuwa 60, na 39.8% ya kura za Lowassaalizopata kwa desilimali ya karibu itakuwa 40. Kwa hiyo CHADEMA imeinya`anyaCCM 20% ya ruzuku, je! Siyo maumivu hayo?

4. Uongozi wa halmashauri ndiyo usiseme. Kabla yaLowassa halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na wapinzani zilikuwa 5 sasahalmashauli hizo zimeongezeika na kufika 30, katika halmashauri hizo CCMwatakuwa bachbancher.

5. Kilio kikubwa zaidi ni cha Zitto Kabwe alichowapaCCM katika halmashauri ya Kigoma/ujiji. Katika halmashauri hii hakuna mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa kutia pua, halmashauri hii ni mali ya Zitto Kbakwe kwamaana ya Meya hadi madiwani. Halmashauri hii mwenyekiti wa CCM au mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa wataenda kufanya nini? Wakati wakuu hao wameng`ang`anakumnyang`anya Kafulila ubunge wake huku nyuma Zitto anachukua halmashauri ya mjini,shame on them

6. Kuna kilio manispaa ya Mtwara/Mkindani na Mtwaravijijini kwa Hawa Ghasia, huenda Umeya wa Shilingi na wa Ndazigula umeotambawa.

Haya ndo ilitakiwa Mh. January Makamba ayaseme katika kile kikao chawaandishi wa habari alichokiitisha.

Source: ebaeban/Jamii Forums

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SO WHATTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTT?

    ReplyDelete
    Replies
    1. TUNAJIFARIJI. MSITUFANYIE HIVYO JAMANI.
      KUFUNGWA TWAFUNGWA LAKINI CHENGA TWAWALA.

      Delete
  2. Muhimu kwetu ni 'U-PREZIDAA' basi; kama ni ubunge hata wangechukua majimbo yote poa tu, huoni jinsi wanavyo haha kuhusu URAIS...........MAGUFULI WOYEEEE, itikia tafadhali, MAGUFULI JUU, NDIO, JUU, JUU, JUU ZAIDI........

    ReplyDelete
  3. Mh ama kweli una roho ya jiwe,, unajipa moyo kiasi hicho basi tutaona watu wa kwenye hayo majiji wakiwa matajiri na wengi wao kuondoka ktk umasikini kama mlivyokuwa mkiimba na itakuwa mfano mzuri kuwawezesheni kushinda kwa 87% ktk uchaguzi wa 2020 kama huu mlishinda kwa 62% hahahhh
    Unajua kwa nini mmeshinda au kupata kura nyingi mijini na hasa mijii mikuu?? wakazi wa mijiini zaidi ya 70% hawastahili kuishi mijini kimsingi (naona hukuwepo wakati wa Mwalimu,,,watu hao walikusanywa na kurudishwa vijijni NGUVU KAZI) na wengi wao ni wale wanaoishi ndotoni na ni thugs wote wako mijini kwa kuwa vijijini hawadumu kimaadili ya maisha.
    Kwa taarifa yako na nakuomba uweke kumbukumbu,, huu ndio mwisho wa vyama vya upinzani Tanzania na hivyo njia ya kuingilia mjengoni itabakia kuwa CCM tu njooni huko watafuta mtaji wote mnakaribishwa kwa awamu.

    ReplyDelete
  4. Wewe hata ufai kuwa kada wala mnazi wa Chadema , jibu swali rais ni nani, pili Ccm ina wabunge wangapi na ww unao wangapi pamoja na washenga wako? Nani wamekula fdha za Lowasa na sasa wanaanza mchezo wa kitoto wa kususa kila kitu? waambieni warejeshe fedha hizo kwa mwenyewe na muanze kujipanga upya miaka 25 ijayo. Uwezi kuongoza nchi kwa ahadi za kuwa rafiki wa bodaboda, mama ntilie na machinga, hao ni mambo mambo madogo kimkakati katika kuliongoza taifa. Tuliwahi kuwasaidia kuhusu kupiga vita ukabila, ukanda na udini mkawa viziwi na vipofu sasa mtaisoma namba kutoka angani.

    ReplyDelete
  5. Presha ya nini?Debe lilikuwa rais awe Magufuli mtu wa kazi na kazi ndio imeanza,subiri muone.

    ReplyDelete
  6. Mtaandika sana mwaka huu,mtaweweseka sana,mtakosoa sana tu,lakini mmeambiwa kampeni zimekwisha,RAIS NI JOHN POMBE MAGUFULI na tufanye kazi.

    ReplyDelete
  7. Subirini 2020 CCM Itashinda kwa kishindo safari hii tumechagua tingatinga sio CCM ambayo ilituboa sana kwa hiyo UKIWA hatujui kama itakuwa hai mpaka wa kati huo labda ya mungu ni mengi na ruzuku ya CDM itakuwa 5%

    ReplyDelete
  8. Hahahahahah!!!hapa kazi tu atutaki maneno kama ni mtunzi mzuri nenda akudo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad