Pili kabla ya kushabikia tujiulize JK alianzaje? Alimsimamisha mkurugenzi Muhimbili akamteua Mwanamama! Huyu naye kafanya vilevile au tumesahau?
Yaani kwa kweli mi ninapoangalia hali ya uchumi wa Tanzania, maisha duni ya wafanyakazi, ukisefu wa ajira ukosefu, wa maji safi ni salama karibia nchi nzima!
Namshangaa sana mtu anayemshabikia Mh Pombe kutembea na vyombo vya habari kwenye maofisi!
Kwanza jiulize huko kote alikovamia amehoreshaje mazingira ya utendaji wa wafanyakazi ili kuwapa morally ya kufanya kazi?
Hizi sio zama za dictatorship style ni zama za democratic leadership ambapo ku win minds za wafanyakazi ni kuwatendea vile inavyopasa na sio kuwakimbiza na viboko.
Tanzania tunahitaji kuona wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata mikopo yao kwa ufasaha na kwa utoshelevu.
Tunahitaji kuona wafanya biashara wadogowadogo wakiboreshewa mazingira ya kazi..mfano mama ntilie na bodaboda na machinga,
Tunahitaji kuona wakulima ambao ndo uhai wa Taifa wakiboreshewa zana za kilimo na mbolea.
Tunahitaji kuona michakato ya viwanda ikianza.
Tunahitaji kuona waalimu wakiimarishiwa mishahara yao pamoja na kulipwa malimbikizi yao.
Tunahitaji kuona jiji la Dar likiokolewa kuondoka na uchafu unaosababisha vifo vya watanzania kila kukicha.
Nina mengi sana lakini ngoja nitulie kwanza, hebu jiulize vijana hawana ajira iko wapi mikakati ya viwanda?
Huko Muhimbili mkurugenzi anasimamishwa kazi wakati tunaona madactari wanagoma kwa mishahara duni iko wapi mikakati ya kuwaboreshea mishahara yao ili kuwapa ari ya kufanya kazi?
Mi nadhani cha kufanya kwa sasa kuboresha kwanza mazingira ya kazi alafu kazi ya usimamizi itakua nyepesi.
" Ukitaka Punda akubebee mzigo vizuri bila kipigo mpe majani na maji ashibe"
WEWE ULIYETOA MADA HII UNAIJUA VEMA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA WIZARA ZA AFYA? NA JE MH. RAIS AMEFANYA KOSA GANI KUHIMIZA MASHINE ZITENGENEZWE NA WATANZANIA WALIO MASKINI KUPATA HUDUMA? AU UNA AJENDA YAKO YA SIRI? VIWANDA VITAANZA KWA SIKU MOJA?
ReplyDeletePesa za repair na maintenance kama zilikuwa hazitolewi na hazina, je mkurugenzi angatoa hela zake mfuko kutengeneza hizo ct-scan na MRI. Hiyo haitoshi muhimbili ina pokea wagonjwa wengi sana inahitaji mashine za aina hiyo zaidi ya 5 ili wagonjwa waweze kupata vipimo kwa makati. Hata ikitokea fault mashine moja au inahitaji normal maintenance nyingine zitaendelea kutoa huduma. Ushauri JPM punguza hela ulizokua umetengewa kwa safari nunua mashine 2 next year na mwaka unaofuata 2 tena. Vile vile na hospitali za mikoa zipate machine hizo. Tukifanya hivyo tunaweza okoa maisha ya watz waliowengi.
DeleteRoho inakuuuummaaa ukiona JPJM anasifiwa ha ha ha utakufa nacho kijiba cha roho!!
ReplyDeleteHuyu ndio RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA utake, usitake........
Hatuna ugeni nayeye, utendaji wake tunaufahamu ndio maana tumemchagua............
Kawaambie walokutuma, it is TOO LATE, kampeni zimekwisha, hivi sasa ni utekelezaji ....
TUNAJUA WAPINZANI WA TANZANIA HIYO NDIO KAZI YENU, 'KUPINGA TU' tehe tehe tehe HAPA KAZI TU.....
Usingekua urasimu unaofanyika kwenye hayo maofisi unayosema anavamia unafikiri nchi hii ingekua hivi.? hata mtu alipwe mshahara kiasi gani kama hana nidhamu na kazi sahau huduma bora. Sio kila kitu cha kucrash.....
ReplyDeleteTunajua umeumia sana, inawezekana baba yako mzazi ndo'huyo mkurugenzi alosimamishwa, au ndio wale walofungiwa 'safari za nje'.., lakini hao ndio walotusababishia matatizo yote hayo uloyaorodhosha, lakini mara baada ya huyo 'baba''ako' kutimuliwa, mashine zote Muhimbili zinafanya kazi.....na bado, hiyo ni trailer, mchezo kamili unakuja........mtanuna sana mpaka muombe 'pooh'.....HAPA KAZI TU
ReplyDeleteNCHI HII BILA 'dictatorship style' HAIENDI, HASA KWA WATU WENYE MAWAZO MGANDO KAMA YAKO, MNAOFANYAKAZI KWA MAZOEA, KUINGIA SAA 2 KUTOKA SAA 4, NA POSHO ZA VIKAO VISIVYOKUWA NA TIJA. NDANI YA WIKI MOJA UNATAKA ETI ABORESHE SIJUI NINI NA NINI, HATA MAWAZIRI HAJAWATEUA. MTACHONGA SANA MWAKA HUU, WEZI NA MAFISADI MWISHO WENU UMEFIKA....SHABHASH
ReplyDeleteWapinzania naona mnajitahidi kumkatisha tamaa muheshimiwa, bure mnajisumbua, mlitaka aboronge mpate la kusema, amewafunga midomo kwa MAKUFULI, sasa mna-tapa-tapa. Huyo ndio MAGUFULI bana a.k.a. TINGA-TINGA ametinga IKULU.......ina-uma hiyo, na ku-wachoma-kama-pasi
ReplyDeleteZanzibar Na meno ya tembo Zurich
ReplyDeleteVinginevyo mchezo wa sinemaaaaaaaaaaaaaa
Magufuli
Mnatuchefua sana nyie wenye chembe chembe za chuki, nafikiri tatizo lenu kubwa ni elimu, Magufuli anaangalia yanayoweza kutatuliwa ktk muda mfupi kwanza hivi kwa akili yenu wavuta bangi wa Ukawa tatizo la maji linaweza kutatuliwa ktk mwezi mmoja hata ktk kijiji kimoja, bangi mnayvuta ni kali sana kuleni vizuri msijemkawehuka!!! Muoneni hivyo tu Tinga Tinga msipoangalia 2020 atapa 99.9% na huo ukawa utakuja kuwa UKWE
ReplyDeleteHAPA KAZI TU!!?? BASI PIGA PUSH-UP UKANUNUE MAHITAJI YAKO!! .KAULI MBIU MPYA NI HII :
ReplyDelete"HAPA KAZI ZENYE TIJA TU!
Wapinzani mwaka huu msipomeza wembe cjui
ReplyDelete'Watakula ndimu' in Gwajima's voice
Delete