Huyu Dereva Tax Atanivunjia Ndoa Yangu, Nifanyeje?

Nimekuja kwenu nahitaji ushauri, ni urgent.

Hapo katikati niligundua kuwa Mr wangu ana kimada, tukasumbuana na kugombana sana juu ya hilo, ingawa sikumshika live ila ni wazi kwamba alikua nae, mbali na hilo pia ni mlevi kupindukia.

Nilipoona suala hilo linaendelea nikaona isiwe tabu, nikatafuta suluhisho.

Na mimi nikatafuta mtu pembeni aniliwaze, kuna dereva tax huwa tunamtumia sana kwa shughuli za kifamilia,
Nikaamua kumzawadia penzi huyo jamaa, sio kwamba nilimuanza mimi, bali alikua akinisumbua siku nyingi, hivyo nikaona nimkubali.

Katika mara zote nilizokutana nae (6) niligundua kwamba hajiwezi kabisa, nikaona this relationship is not worth it, nikampiga chini, pia mtu mwenyewe hana hata Chumba cha kulala, Mara zote anaazima Chumba kwa mwenzie, ingawa ukimuona kwa nje ubrazamen alionao huwezi amini, ni type ya wale wanaume wenye kuongea sana na mbwembwe nyingi lakini hamna lolote.

Nikakata mawasiliano nae na kumwambia asinitafute tena, akaanza kunililia nisimwache, anapiga simu muda wote kunibembeleza, kila akiniona hata na watu wengine Mtaani, labda Dukani n.k atakimbia haraka kuja na kuomba tuongee pembeni hadi kero.

Hivi karibuni nimepata mtu mwingine mahali nakoabudu, he is so caring, ni mtu mwenye Upendo sana, hanywi pombe na ananipenda kwa dhati, he is god fearing and above all his performance is much better than my husband and the tax driver's.

Juzi kumetokea shida kubwa baada ya Mr kushika sms ya yule tax driver akiendelea kunibembeleza, Nikalazimika kusema kuwa jamaa ndio ananifuatilia, ananitaka kimapenzi, akasema kama ni kweli na ili aniamini Basi tufanye fumanizi la kutengeneza, kwamba nikubaliane na yule kijana wa tax kwenda nae guest na yeye aje atufumanie na kundi la mabaunsa wamwoe wote.

Nikikataa mpango huo basi atajua nilishatembea nae, na mimi najua yule tax driver kwa vyovyote vile atauvaa huo mtego, namuonea huruma sitaki apate aibu hiyo wakati tulishaachana nae.

Nipo njia panda naombeni ushauri nifanyeje?
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WASWAHILI WALISEMA"HASIRA ZA MKIZI FURAHA YA MVUVI"HIZO TOPE UMEJIKOROGEA MWENYWE SASA KAA MKAO WA KULA UZINYWE MWENYWE KUDADEKI

    ReplyDelete
  2. Kumbuka kuwa ukifanyacho gizani kuna siku kitaonekana katika muangaza watu wakione

    ReplyDelete
  3. duh haya maisha ya mapenzi siyo kabisa, yaani everything ain't real, tax driver anajua Una mume mtishie kwamba mumeo anamtafuta amfanyie kitu mbaya, lzm ataogopa endelea kula bata na mpendwa,

    ReplyDelete
  4. Huyo Wa church mpendwa au Shetani katika vazi la kanisa???? God fearing anatoa mbwa wake za watu??????????

    ReplyDelete
  5. Ww kweri ni paka mweusi uriye jaa pepo chafu la umalaya unatiya kinyaaa

    ReplyDelete
  6. kwa kahaba uliyekubuhu kama ww ngoja yakufike zaidi ya hayo

    ReplyDelete
  7. Enter your comment...kama unakuwa huz kumshaur m2 n kher ukafunga kopo lako la choon m2 kaomba ushaur anaitaj mawazo yamsaidie kusolve tatzo lakn wewe na akr zako nying unatoa lugha isyo stahli iv we umejiumba hujawai kukosea? achen izo bhana so poa hta kdogo assume n wewe yamekukuta huz omba ushaur kwel?,...Pole my dear matatzo haya yanamfka kila alie bnadamu japo hayafanan ila hujatofautitofaut mwambie dreva tax kuwa mumeo keshajua inshu nzma so akae mbali na wewe ucje ukaruhsu ilo fmaniz n hatar kwenu c dreva tax 2 atakae hadhrika hata wewe pia utahadhrika kwan wa2 watajua umwefumwa na mwanaume gest.

    ReplyDelete
  8. Pole sana ndo maisha yalivyo kiukweli kila mtu hukosea. CHa kufanya mtel dreva tax mumeo kanasa ishu na anamtafuta sana asithubutu kukutumia msg wala kukupigia kwani na simu yako mumeo anaimiliki siku hizi. Kutoka nje ya ndoa ni kawaida sana unapokua na matatizo na mumeo hasa ukigundua anakucheat. ucjali yatapita

    ReplyDelete
  9. Worry out dogo yanatokeaga sana hayo sema wengi hawaandiki nikiwa mmoja wapo. Mume wangu mimi alitembea na mwanafunzi hadi kero nami nikarudia mchepuko wangu wa zamani kabla sijaolewa ila sijawai kamatwa mbaya zaidi namleta mpaka home jamaa akiwa hayupo na nilimwambia lazima nimlipize cause huyo mwanafunzi alikua ananitukana sana. So mtel tu dreva asimame endelea na huyo mwingine kama anakupooza maisha ndo haya haya huna haja ya kuumia kimapenzi kwani mungu yupo nawe hata yeyey anavyozini anajua mungu yupo na yeye ndo chanzo cha wewe kutoka nje ya ndoa.

    ReplyDelete
  10. Chery hujaolewa? nadhani wewe sio mshauri mzuri

    ReplyDelete
  11. Inavyoelekea unapenda kufungua zipu tofautitofati hats ukisema Na akili yako Leo mwisho moyo utasema kesho ndio mwisho tatizo lolote la ndoa siyo cheating unatakiwa litatue Na mwenzio

    ReplyDelete
  12. Pole sana dear, mitihani ya ndoa huwa ni mingi sana. Wengi hujikuta wamechepuka bila kutarajia. Unakuta mtu unyumba hakupi, kipigo wakati unahuzunika anatokea mfariji na kumbuka wakati ukiwa na matatizo faraja ndiyo sehemu yake, wajikuta ushateleza. Nakushauri umwambie huyo dereva tax kuwa mumeo ameshajua, na anataka kufanya mpango ili mfumaniwe na afanyiwe kitu mbaya. Pia usikubali kutengeneza hilo fumanizi, kwani moyo wa mtu kichaka, ukute alishakuchoka ndiyo maana anakufanyia visa vilivyopelekea nawe kuchepuka, utakapofanya hilo fumanizi la kutengeneza kwake laweza kuwa kweli na ukawa ushahidi tosha na kuwa ndiyo ticket yako ya kurudi kwenu.

    ReplyDelete
  13. hivi nataka kujua jambo. hapo juu inasomeka kuwa your comment will be visible after approval. So hata hiyo lugha ya matusi huwa inakuwa approved ndiyo inatumwa?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad