Jack Wolper Adai Hakika LOWASSA Ni Shupavu na Jasiri Haijawahi Tokea

Jackline Wolper
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Jacqueline Wolper, aliyekuwa mstari wa mbele kumsapoti mgombea urais kwa mwavuli wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa, amedai kuwa kwake yeye mheshimiwa huyo ndiye kiongozi shupavu na jasiri.

Wolper, amemmwagia sifa lukuki waziri mkuu huyo wa zamani na kuwataka Watanzania kuwa pamoja katika kuijenga nchi na kudai kuwa Mh. Lowassa amekuwa mstari wa mbele kwa kupambana kwa kuleta mabadiliko kwa watanzania.

Amenukuliwa akisema kuwa anaamini kuwa Lowassa, ameleta historia kubwa sana nchini kwasababu haijawahi kutokea Tanzania, kwani ametuma ujumbe kwa viongozi wengine ambao walikua wazembe na waliojisahau na kudai kuwa anaamini wataifanya nchi kuwa mpya.

Ameongeza kuwa yeye bado anaamini Lowassa ni kiongozi shupavu, muelewa na mwenye akili za kupambanua mambo, na kusema kuwa kushindwa kwake haijalishi kwa sababu anaamini watanzania wanamkubali hasa kwenye mabadiliko.

Aidha, amewataka wasanii wenzake ambao wapo CCM wasijengeane chuki kwa yaliyotokea kwani aliamua kutafuta haki yake ya msingi akiwa kama msanii.

Sambamba na hilo amedai kuwa kwa wana mabadiliko wenzake waendelee kupambana na watakao wawakilisha bungeni wafanye kazi ya maana hasa kuwatetea wanyonge.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JACK WOLPER WW NI MJINGA VIPI UNASEMA LOWASA NI JASIRI HUYO NI MWIZI MKUBWA

    AU TUSEME UMEMPA KITUMBUA CHAKO NDIO MAANA UNASEMA SHUPAVU WW ENDELEA

    NA KAZI ZAKO ZA KILA SIKU MALAYA MMOJA


    ReplyDelete
  2. Kweli ni jasiri na shupavu, maana bila ujasiri huwezi kujinyea jukwaani na bado ukaendelea na kampeni, mara anapoteza network lakini yumo tu, kweli huyo babu ni jasiri si mchezo, yeye na mkewe wote ni majasiri, angekuwa mwanamke mwingine asingekubali mumewe adhalilike kiasi kile, inataka ujasiri....hongera zao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad