JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje Kushinikiza Maalim Seif Atangazwe Mshindi wa Urais Zanzibar?
Toa Maoni yako
JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje ?
36
November 20, 2015
Tags
huyo anajulikana!! hilo c swali!!
ReplyDeleteYule si mwanaccm. Hamuoni hata Jinsi ushindi wake ulivyokuwa rahisi wakati wabunge wengine wa CDM, CUF, NCCR wakilazimika kulinda kura zao na kupambana kweli kweli ili watangazwe.
ReplyDeleteZZK ni msaliti wa watanzania, hana Jipya
You said it all..
DeleteHausiki na UKAWA! Angebaki Mbatia au Lissu ndo ungehoji kwanini!? Hivyo hawezi kuingilia mambo yasiyomhusu.
ReplyDeleteKwani Zitto ni UKAWA?
ReplyDeleteWALE WOTE WANAOTAFUTA AJIRA INGIA HAPA : http://newjobstz.blogspot.com/
DeleteUkimuona mtu katika ugomvi wa (man to man) mtu kwa mtu yeye anakimbilia silaha ujuwe si mpiganaji ni mhalifu. Kukimbilia vurugu kwa ukawa badala ya kukaa na kupambana kwa hoja za msingi inaonesha jinsi gani walivyojiegemeza katika kutengeneza migogoro zaidi kuliko amani. Zito ni mweledi na mwenye nia ya dhati ya kuweka utaifa kwanza chama baadae.
ReplyDeleteANA AKILI TIMAMU HIZO KENGE NDO TUMEZITUMA ZIKAPIGE KELELE BUNGENI, HUKO NDO KUTUWAKILISHA?
ReplyDeleteNi sawa Tu, walitoka Ni ukawa na waliobaki Ni ccm.
ReplyDeleteWe hujui hata kutodautisha zitto ni ACT waliotoka ni CUF,NSSR,na CDM hao ni UKAWA kwahiyo zitto na chama chake wana utalatibu wao na hao wanao jiita UKAWA wanataratibu zao pia hivyo usilazimishe mtu aige ige tu ovyo mswahili alisema usiige kunya kwa tembo
DeleteZITTO NDIYE ALIYESEMA ZANZIBAR HAKUNA RAISI, AU SIYO JAMANI? LEO HII AMESHAKUBALI ZANZIBAR KUNA RAISI AU....
ReplyDeleteCheck link hii ujue alichosema kuhusu uraisi zanzibar: http://niajetz.blogspot.com/2015/11/zitto-vs-president-of-zanzibar.html
Zito hana uzito mwache akae tu bungeni, anatimiza zile alama za unafiki
ReplyDeleteNi kukua kisiasa tena anahekima ya hali ya juu amewatendea haki wananchi wa jimbo lake
ReplyDeleteWazanzibari ni Watanzania. Inawabidi Watanzania wote kutatua tatizo la Zanzibar kwanza kabla ya kufanya chochote. Hamuwezi kulikwepa. Zito hawezi kuleta maendeleo Kigoma kama serikali inayumba. Ni upumbavu na ujinga mkubwa kujidanganya. He is a Hippocrates.
DeleteWatu mnashindwa kuelewa. Zito hana siasa za ukawa wala hashiriki vikao vya ukawa. Zito anachama chake na sera zake. Kukaa bungeni haimaanishi kwa anakubaliana na yanayotokea zanzibar. Kama msomi na pia mwanasiasa alishatoa mchango wake wa kimawazo na misimamo kuhusu uchaguzi wa zanzibar. Katimiza wajibu wake. Lkn hakuwahi kusema Kama aliyoyasema hajafanyiwa kazi eti atatoka bungeni. Zito c kiongozi wa migomo. Zito ni kiongozi wa hoja tena zenye maslahi mapana ya kitaifa. Kama wenyemamlaka wameamua kuukandamiza uchaguzi wa zenj wengine hata mngefanyeje ni shida tu. Mnaona leo police yote na magari ya kuwasha wamehamia dodoma. Eti kuwapiga wabunge. Hii inathibitisha ubabe wa watawala na viburi walivyonavyo. Wajibu wetu ni kusema hasa ktk mambo Muhimu kwa taifa. Ukawa ilifahamika wazi wangetoka hata si tu kwa sababu ya zanzibar, ingepatikana sababu nyingine. Mwacheni zito afanye kazi na wajibu wake. Na haina maana kumwita msaliti. Wasaliti kwenye siasa halieleweki.
ReplyDeleteWananchi wakimchakua mbunge wanategemea atawatetea kwenye sera zoa,sio kukimbia na kutoka bungeni,inawapasa wabunge wazungumze matatizo ya watu waliowachagua,ikiwa wantoka bungeni ni waoga na mishahara wasipate.
ReplyDeleteMsimbazy
Wachaga waliona uwezo wa zito kwenye chama ni tishio wakaamua kumtumua na kusambaza taarifa za usaliti. Mm namshauli hata mbatia angehamia tu chadema ili nccr wajijenge upya. Usaliti wa zito uko wapi. Hivi zito, slaa Ndo wakulinganishwa na edo au mbatia. Acheni mambo yenu ya kutafuta zito. Mlimtimua mlizani kaisha kisiasa. Zito ni jembe watanzania tunamtaka na atafika mbali na chama chake.
ReplyDeleteSimamia Taifa. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Nyinyi msioona mbali na kujua madhara ya jambo hili. Hamtaweza kuelimika hata. Ni watu kama nyinyi tatizo na mzigo duniani. Hamna mapana. Narrow minded people.
DeleteZito atoke nje ye kwani ukawa, SI walimfukuza cdm sasa kwanini Leo awaunge mkono ilhali yeye kkaingia bungeni kwa tiketi ya act na sio cdm na act haipo ukawa, safi Sana zito big up endelea kuwakilisha wanakigoma, shame on them wabunge wote waliotoka nje, wagome na posho basi, safi Sana ndugai umefanya kitendo cha kishujaa kuwatimua, hivyohivyo adi wanyooke
ReplyDeleteZITTO ANA AKILI SIN SAWA NA HAO UKAWA WASIO NA AKILI
ReplyDeleteFikra finyu.
DeleteNdugu sikuwa na nia ya kukujibu,ila hujaeleweka umetumia lugha gani.Fanya marudio ya ulichoandika kabla ya kupost.
ReplyDeleteLABDA AJE AONGEE YEYE MWENYEWE.NI WAZI BAHASHA NZITO IMETUMIKA.HII NI AIBU NA FEDHEHA KUBWA KWA ZITTO MBUNGE PEKEE WA ACT BUNGENI,CCM HAWAJACHOKA,WANANUNUA UTU NA HESHIMA BUNGENI WAMEMVUA NGUO ZITTO.PESA CHAFU ZA CCM BADO NI TATIZO ZINAGAWIWA KAMA NJUGU NA ZITTO KAMEZWA.AIBU,AIBU,AIBU,NI WIZI MTUPU,WIZI!
ReplyDeletezitto maskini,kaelemewa na bahasha nono ya ccm,kajivua utu kwa pesa.kamkosea muumba wetu,adhabu ya wasaliti ni moto wa dunia na jehanamu.bahasha ya january na nape zimemtoa utu.fedheha,aibu,uchafu.
ReplyDeleteNi mwana ccm kwa mlango wa nyuma
ReplyDeleteNilichotaka kuongea ni hiki. Wazanzibari ni Watanzania. Bila wao hakuna Tanzania bali Tanganyika na Zanzibari. Sasa Watanzania tunapowadharau Wazanzibar, tunaposhindwa kupigania haki za wenzetu wa Zanzibar, Tunaposhindwa kufuata demokrasia, Tunapopindisha sheria makusudi na kuadhibu watu, Huu ni uonevu, huu ni uharamia, huu ni uhujumu, matumizi ya nguvu yanayoonekana wazi lazima Watanzania wote tuungane na kuyakataa pamoja. Sasa kama Raisi ni wa Muungano utatawala namna gani ikiwa hujali vilio vya wananchi. Utawapuuzaje ukitegemea uwe kiongozi. Je kama unamsimamo huru wako binafsi bila kupandikizwa na Raisi aliyeamua kukuachia mzigo si wako. Kwa nini usiukatE.kAMA ccM INANIA YA MABADILIKO KAMA ILIVYOSEMA Kabla ya uchaguzi. Je haya ndiyo hayo mabadiliko? hii ni misukosuko. Je kama Mlimwamini Magufuli kwa uchapa kazi, Je atachapaje kazi kwa kuigawa Tanzania? Kwa nini Watanzania kama binadamu mnashindwa kuwa na vionjo na kuumia kama mwenzio anaumia. Magufuli ameambatana na raisi aliyepita na kushindwa kumtangaza Raisi ambaye Wazanzibari kwa kutumia kura wamemchagua. Watanzania ni Wajinga kiasi gani kukubali kuburutwa na chama kongwe hata kwa bunduki na kukaa kimya. Ilibidi nchi nzima iiandamane kuwaunga mkono Wazanzibari. Nashangaa jinsi sisi watu wa bara tulivyo waoga, mbumbumbu, na ni mainfirio kutokuweza kusimama na kudai haki zetu.
ReplyDeleteInashangaza tunasifiwa kwa amani na mtu aliyepewa zawadi kwa kudumisha Amani kashindwa kuleta amani nyumbani kwake. Ni hawa mabwana wenye maslahi nchini wamembeba kuhifadhi maslahi ya wizi. Je huu ndio udemokrasia wanaouleta Tanzania? Je Watanzania hajui demokrasia ni nini. Je Kwa nini mnapiga kura, Kwa nini mmekubali vyama vingi kama chama gogo ni dictata.
Na zitto simfahamu msimamo wa bwana huyu nduma kuwili mpiga kelele aliyebaki bungeni lakini alitoa kauli ya kumambia Magufuli amtamke raisi aliyeshinda. Kajibwedeka pale. Kijana ndumila kuwili ni huyu. Wazanzibari ni ndugu zetu, Kwa nini mnawaacha kama Wanyama.
Zito anateteya maslayi ya inchi siyo maslayi ya ukawa
ReplyDeleteZitto si mtu wa kufuata mkumbo ana uelewa wahali ya juu amelinda heshima zake kuliko hao vibaka (ukawa) wangepingakwa hoja tungewaona sana wa maana lkn mpaka hapo mazombii
ReplyDeleteWEWE UNAYESEMA ZITTO KAPEWA BAHASHA NA CCM UNA UHAKUKA GANI WA UNACHOKIONGEA, NA MOTO HUO UTAWAWAKIA, MUNGU SIO WA KUCHEZEWA. MLITAKA KILA HATUA YA KUTATUA MGOGORO WA ZANZIBAR MUAMBIWE NYINYI KAMA NANI, WAKUBWA NDIO WANAJUA WAMEFIKIA WAPI KATIKA SWALA LA ZANZIBAR.
ReplyDeleteSUALA LA ZANZIBAR NI LA WATANZANIA WOTE UKISEMA MKUBWA SIJUI UNAMLENGA NANI ?
DeleteZito Kabwe anajitambua, hawezi kuingilia mambo yasiyo na maana. Zito anamuhitaji Magufuli kwa ajili ya jimbo lake, hata wafanye nini ni LAZIMA narudia LAZIMA wapeleke shida zao kwa serikali hiyohiyo kwa ajili ya majimbo yao. Sawa, ukawa wametoka......THEN WHAT??? Bunge liliendelea au halikuendelea???? WAJIPANGE UPYA.........HAPA KAZI TU
ReplyDeleteKAMA SUALA KUBWA LA ZANZIBAR UNAONA HALINA MAANA NINA MASHAKA NA UPEO WAKO WA UELEWA WA MAMBO
DeleteZitto anaelewa. Bunge ni chombo cha kutunga na kupitisha sheria. Na anaelewa kuwa serikali yetu Ina mihimili mitatu ambapo kila mhimili Una kazi yake. Mihimili mingine Ni chombo cha kusimamia utekelezwaji za sheria zilizotungwa na mhimili wa mwisho Ni chombo cha kutafsiri sheria inapokosewa. Akiwa mbunge aliyechaguliwa na wananchi wajibu wake Ni kufikisha kilio cha matatizo yetu watanzania ktk bunge letu ili yapatiwe ufumbuzi nasi tusonge mbele. Naamn ,kila mambo limo ndani ya sheria. Na kama Kuna mambo linaonekana kukandamiza wananchi kisheria, naamn ktk vikao vyao basi waliwasilishe ili hiyo sheria kandamizi ifanyiwe marekebisho au ifutwe. Ni kweli tunaiga mabunge ya nchi zingine. Lkn SI kila kitu Ni cha kuiga. Tusipojiangalia tutaiga hata sheria za kuruhusu ushoga na tutaona Ni hali yetu kuiga. Hii ya kuiga vurugu za mabunge ya nje, hamuoni ni kutufundisha ss tulioko majimboni tabia za ajabu ajabu? Unategemea nn kwa mtanzania ambaye atafanyiwa uhalifu? Adai haki yake kwa kukusanya wapendwa wake na kumfanyia vurugu? Mkumbuke wanaoliangalia bunge ni watanzania na kila binadamu Ana tafsiri tofauti kwa mambo analoliona mbele yake. Hilo ni bunge letu sisi. Wazanzibari wana bunge Lao. Na siku zote wamekuwa wakigombana na kuwekana sawa wenyewe. Waachieni matatizo Yao watayamaliza wenyewe. Hapo bungeni mmeenda kututetea sisi na kutuletea maendeleo wa tz. Kuna vyombo vingi kimataifa vyenye uwezo wa kusimamia migogoro ya Zanzibar endapo wazanzibar watashindwa kuitatua ki region.kuna OAU, UN, nk. Demokrasia zingine zitatuingiza kwenye tuvikundi twa kudai haki like Boko haram. Fanyeni tulichowatuma bungeni.
ReplyDeleteUmeanza vzr lakin huku mwishoni nadhani hauko sawa mkuu, Zanzibar ni part ya Tanzania na ndio maana hata kabla ya JK kuondoka madarakani tulihitaji ashughulike na hili tatizo, kinachoendelea Zanzibar kila mtu anakijua, unaposema matatizo ya Znz watatue wenyewe hauko sawa kabisa. ccm wanapora ushindi kila mtu anaona kama kweli watz tunahitaji maendeleo ya taifa letu kiujumla tuacheni siasa za kivyama
Deletemnao muunga mkono zito wote hamjielewi!! ndio nyie mliunga mkono JPM kuvamia muhimbili bila kujua source ya tatizo ni nini!! mkamkashifu alyetolewa kumbe mwisho wa siku tatizo ni hazina wanadaiwa bilioni saba!! na hili hajalipima kwa makini kumbukeni siku ile kulikuwa hakuna kuchangia hoja bali rais kuhutubia bunge, na wao walimpa masharti kuwa shein hasiende kwani siyo rais tena waznz muda wake umekwisha!!! na kama anaenda basi awe kama mgeni mualikwa asipewe itifaki za kirais, lakini bunge likampa itifaki za kirais ambazo zilitakiwa ziwe za Maalim!!! ndipo hapo ili kuonyesha dunia ccm inachofanya sicho ndio ukawa wakaamua kufanya vile walivyofanya. na ni haki kwani si walikuwa wanaonyesha hisia zao ni kiasi gani hawakubaliani na mambo yanavyoendelea nzn!!! sasa kosa lipo wapi hata muanze kuwaona hawafanyi kazi waliotumwa na wananchi!!???
ReplyDeleteKuhusu swara la Zanzibar mh zitto mbona kishalitolea ufafanuzi we upo nchi gani? Tena alieleza kisheria na kikatiba ya Zanzibar
ReplyDelete