Jeshi la Polisi limepiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa na Maandamano

Jeshi la Polisi nchini hapa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa kwa kile ilichoeleza tathimini iliyofanywa na jeshi hilo inaonyesha bado kuna mihemko ya kisiasa ambayo inaweza sababisha uvunjifu wa amani endapo itaruhusiwa kufanyika.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini ssp Advera Bulimba, amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa, maombi yote ya kufanya mikutano na maandamano yaliyotolewa na vyama vya siasa vya CCM na Chadema yamezuiliwa mpaka hapo hali itakapotengamaa baadae.

chanzo. Chanel 10


NIONAVYO:Hii inamaanisha nini kuhusu kampeni za uchaguzi mdogo,kuwa kampeni hazitatumia mikutano ya kisiasa?

Hao watu wenye mihemko wapo kiasi gani? Na kwa nini wanamihemko? Kwa sababu wameshinda au kushindwa au kudhulumiwa?

Ningeshauri polisi wetu waendeleze weledi waliouonesha kwenye kulinda mikutano ya kampeni kwa kuwaruhusu watu waandamane au hata kufanya mikutano ili kuwaondolea msongo na kuanza maisha mapya kwa #HapaKaziTu.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msago jamani
    CCM hiyo yote rukhusa

    ReplyDelete
  2. mimi sioni kama kuna haja ya kuendelea na siasa ya vyama vingi nchini tanzania.sasa hivi ni utawala wa chama kimoja ccm na wamewakabidhi polisi nguvu na mamlaka ya kuisimamia nchi kidola.hapa hakuna demokrasi tena.hauruhuswi kujumuika kisiasa,kufanya mikutano na au kuandamana hata kama utatoa taarifa ya miezi sita kabla.sasa hivi polisi si tena kwa ajili ya usalama wa raia ila POLISI YA UTAWALA HUU WA AWAMU YA TANO NI KWA AJILI YA USALAMA WA CCM.huu ni ukatili wa daraja la juu,ni kuvunja sheria nyingi zaq haki za binadamu.wananchi tumekwisha katishwa tamaa na tabia hii mpya ya jeshi la polisi kuwasakama wananchi wasio na hatia badala ya wahalifu.mitaa imesheheni maaskari wenye zana hatari za kivita,wamenuna kama sio raia wa tanzania wanaranda kuwatafuta chadema badala ya kuwatafuta na kuwakamata wezi,vibaka,na majambazi wa siasa wanaofahamika na wote -CCM.POLISI MNATUMWA,SAWA,LAKINI MNATIA AIBU KUBWA SANA KWA RAIA WEMA.kama utawala wa magufuli utaendeleza maonezi haya ya polisi basi nvyema ikapelekwa decree bungeni ipitishwe kuidhinishwa turudi kwenye MFUMO WA CHAMA KIMOJA.KWA MFUMO HUU WA UKANDAMIZWAJI UNAOFANYWA NA POLISI kwa kuwapiga wananchi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad