Job Ndugai Aanza Kuweweseka...Adai Tutegemee Migomo ya Hapa na Pale Katika Bunge Lijalo...Kisa Hichi Hapa

Baada ya kuteuliwa na CCM na kupita katika mchakato wa kumpata mgombea Uspika wa Bunge la Kumi na moja bila kupingwa, Job Ndugai ameeleza changamoto anazotarajia kukutana nazo ikiwa ni pamoja na migomo.

Akiongea na waandishi wa habari jana baada ya jina lake kupitishwa, Ndugai alilielezea Bunge la kumi na moja kama Bunge lenye utofauti mkubwa na mabunge mengine huku akidai kuwa ongozeko la vijana wengi na wasomi wengi zaidi kunaashiria kuongezeka kwa changamoto zaidi.

“Bunge hili lina wabunge wengi vijana, lina wabunge wengi wasomi zaidi kuliko mabunge yote yaliyowahi kutokea na lina uwakilishi mkubwa. Hili ni Bunge ambalo litakuwa na changamoto nyingi, tetegemee migomo ya hapa na pale, hata hivyo ubora wa kazi utakuwa mkubwa,” alisema Ndugai.

Hata hivyo, Ndugai alisisisitiza kuwa ataliongoza Bunge kwa weledi na kutenda haki kwa kila upande hivyo aliwataka wabunge wote wakiwemo wa upinzani kumuunga mkono leo ili awe Spika wa Bunge la 11.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni ndoto kubwa. Kazi imekuzidi uwezoo wasomi ndio wanaokuogopesha au uwezo mdogo. Jitafakari kama unaimudu hiyo kazi kweli. Au usiikubali. Bunge ni kioo cha n hi.

    ReplyDelete
  2. huyu bwana hakufaa kabisa kuwa spika

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad