Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited(SBL) Stanley Samtu (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (Kushoto) ni Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija na (kulia) ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL), Stanley Samtu (kushoto), Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (kulia) na Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez (katikati) wakionyesha bidhaa mbalimbali za Johnnie Walker wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (wa kwanza kulia) na Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez (katikati) kwa pamoja wakiwa na mabalozi wa pombe kali ya Johnnie Walker Chiku Ally(wa kwanza kushoto) na Judith Mbowe(wa pili kulia) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
Chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries “Johnnie Walker” imezindua kampeni mpya iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” siku ya leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ikiwa na lengo la kuwahamasisha watu kuwa na furaha katika kila wanachokifanya kwa vile furaha huleta maendeleo na sio kinyume chake kama wengi wanavyodhani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Kampeni hiyo katika hoteli ya Serena, Mkuu wa kitengo cha Masoko pombe kali wa Kampuni ya bia ya Serngeti (SBL) Stanley Samtu alisema “Kama chapa, Johnnie Walker imesimama daima kwenye upande wa maendeleo. Imekuwa hivyo kwa miaka takribani 200 tangu mwanzilishi Johnnie Walker alipoanza ufundi wake. Uzoefu umetufundisha kwamba maendeleo hayatakiwi kuwa safari ya kupanda tu na isiyo na kikomo bali tunaweza kupiga hatua na kufurahia katika malengo tunayoweza kuyafikia kila kukicha. Hiyo ndio maana halisi ya kampeni hii ya Furaha itakufikisha mbali zaidi”.
Kufurahia kile unachokifanya ni sehemu kubwa na muhimu ya kufanikiwa na kuwa na maendeleo. Katika juhudi za kufikisha ujumbe kwa wahusika, Johnnie Walker inategemea kuwamulikia baadhi ya nyota katika fani mbalimbali waliojizolea umaarufu kutokana na mafanikio walioyafikia. Hawa ni pamoja na Sheria Ngowi wa tasnia ya mitindo, Dj Frank Jez kutoka Ireland na Dj Peter Mo. Vijana hawa wote wamebobea katika kile wanachokifanya na wamekuwa mfano wa kuigwa nchini. Wamekuwa sehemu ya dunia ya watu ambao wanaaamini kuwa chanya siku zote katika kazi ni moja kati ya vitu viliyowasaidia kufika mbele zaidi katika fani zao.