Julius Mtatiro Afunguka Kuhusu kesi ya Kupinga Ushindi wa CCM Segerea

Napenda kutoa taarifa hii rasmi na ya awali kwa wananchi wa Segerea na watanzania wote ambao walipigana kufa na kupona ili kuhakikisha UKAWA tunashinda madiwani, mbunge na kuongoza kura za Rais hapa jimboni. Kwa bahati mbaya tulifanikiwa kushinda madiwani wote, kuongoza kura za Rais lakini tukashindwa kwenye Ubunge.

Baada ya jimbo letu kwenda CCM nilishauriwa nisisaini kukubali matokeo na nikatekeleza ushauri huo, lengo lilikuwa ni kuwapa muda wanasheria wetu na mawakili waweze kushauri ikiwa kuna kesi ya kufungua kupinga ushindi wa CCM.

Baada ya mashauriano ya wiki kadhaa yaliyohusisha mawakili na wataalam wa sheria wa ngazi mbalimbali, tumejiridhisha na kushauriwa kwamba hatutakuwa na kesi ya kufungua, na kwamba tukiifungua kwa kulazimisha au "kwa kusukumwa na upepo wa wananchi" tutashindwa mahakamani mapema.

Wanasiasa wengi hukimbilia mahakamani wanaposhindwa uchaguzi si kwa sababu wana kesi zenye ushahidi wenye mashiko, bali huogopa maneno na tuhuma wanazoweza kupewa kuwa "wamenunuliwa na wagombea wa CCM", mimi kwa bahati nzuri sijakumbwa na upepo huo na natambua wananchi wa Segerea wananiamini kiasi cha kutosha.

Baada ya wiki moja kutoka sasa, ntatoa taarifa rasmi na ya kina juu ya hoja na sababu zilizopelekea wanasheria na mawakili wetu washauri tusihangaike kufungua kesi na kupoteza muda wa matumaini ya wananchi.

Mtatiro Julius,
Segerea.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chadema ndio walokuponza kwa tamaa yao, ungesimama peke yako ungeshinda, lakina chadema nao wakamsimamisha mgombea badala ya kum-support mgombea mmoja. Nakuunga mkono usipoteze muda wala pesa yako eti kupinga matokeao, HAYO WALIYATAKA CHADEMA AMBAO WAPO KWA AJILI YA KUWABURUZA WENZAO KWA KILA KITU.............POLENI SANA CUF, NLD NA NCCR, MMEPIGWA 'CHANGA LA MACHO'

    ReplyDelete
  2. ni aibu kupinga matokeo kwa ubunge wa ndoa, yani muungane wawili mwenzenu mmoja anawashinda ha ha ha.

    ReplyDelete
  3. Tuko pamoja kaka. Haina haja. Tufanye mambo yenye faida kwa taifa. Hilo liko wazi kura zako na za cdm zinaitoa ccm. Sasa shida iko wapi.mlishinda upinzani lkn tume haiwezi kujumlisha matokeo ya vyama viwili Halafu imtangaze mmoja.

    ReplyDelete
  4. roho imekuuma kukosa ubunge, unachonga sana unaonekana bado una kinyongo na mabosi wako kama vipi amia act-wazalendo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad