Kafulia Afungua Kesi Mahakama Kuu Kupinga Ushindi wa CCM.......Tundu Lissu Ajitosa Kumtetea

Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR -Mageuzi, David Kafulila, amewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kupinga ushindi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasna Mwilima.

Akizungumza na mtandao huu jana baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Kafulila alisema amefungua kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015 ya uchaguzi, akiwalalamikia Mwilima, msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Alisema kesi hiyo itasimamiwa na mawakili wawili, Tundu Lissu na Daniel Lumengela, huku hoja ya msingi katika shauri ikiwa ni kupinga matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi ambayo anadai si halali kwani kutokana na fomu 382 za vituoni na kusainiwa na wasimamizi na mawakala, alipata kura zaidi ya 34,000 dhidi ya 32,000 za mpinzani wake (Mwilima).

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nisingemshauri kuchukua uamuzi kama alioufanya, kwani atapoteza pesa zake bure.

    ReplyDelete
  2. kafulila acha tamaa hujtosheka tu, haikuwa riziki yako waachie na wenzio ubunge ni kupokezana kijiti wala uwezi kushinda. aliyetangazwa mshindi mkubali na umpe ushirikiane. kwa nini ukubali kuwa kura hazikutosha, wananchi wamemchagua mwingine. tulia angalia ustaarabu mwingine. wananchi sasa tumeamka km hukutujali tunakubwaga tu. kipi ambacho ulichokifanya jimboni hadi tukurudishe. kazi yako ilikuwa kurumbana na ccm tu hukuwa na la maana ndio maana tumeng'oa kafulila.

    ReplyDelete
  3. anahera za kuchezea huyo

    ReplyDelete
  4. Jamani.... Kaka pole.. tena pole Sana.. ni nataka ya with.. omba mungu akupe uhai na afya Inshaalah ujaribu tena bahati yako.. kipindi kijacho. CCM imetulea na tumekuwa Unayo.. Itakupa so busara kuanzisha mbio ambazo hatima YAKE utaambulia patupu.. usibugi step.. Ni Wrong namba ndugu Yang... wewe kubali Halafu jiandae na kujizatiti pindi kijacho

    ReplyDelete
  5. Kama una ushahidi wa kutosha kupinga matokeo ni haki yako kufanya hivyo. Uskubali mtu yeyeto akukatishe tamaa umelisaidia sana taifa kuhusu wizi wa Escrow. If its the wilL of God u will win the case my dear brother. Ni ajabu kwa mtu aliye tayari kupigania nchi yake kufa na kupona eti kakataliwa na wananchi!!! Haiingii akilini endelea kupambana bro'.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad