Kasi ya Magufuli kiutendaji itasababisha kudhoofika kisha kufutika kwa UKAWA Katika Ramani ya Siasa Tanzania

Tangu aapishwe kushika madaraka kama raisi wa awamu ya tano, Raisi JP Magufuli amekuwa na kasi ya utendaji wa ajabu.

Amekuwa akifanya yale mambo yanayowagusa wananchi wa kawaida wa chini. Hili limemfanya kujijengea umaarufu mkubwa kwa wakati mfupi tu.

Sio siri mashabiki wa CCM na UKAWA kwa pamoja wamekiri kuwa huyu ndo raisi tulokuwa tukimhitaji. Mitaani, makazini, kwenye mikusanyiko habari ni Magufuli tu.

Amenoga ile mbaya! Kasi hii ya Magufuli Kiutendaji itasababisha kudhoofika kisha Kufutika kabisa kwa UKAWA kwani hata baadhi ya wana ukawa wanasema hakuna haja ya taifa letu kupoteza fedha kwa ajili ya uchaguzi 2020 Magufuli aendelee tu hadi 2025 ili ainyooshe nchi.

Wengine wameshauri pia mgombea wao bwana Lowassa arudi tu Monduli kuendelea na ile kazi aloiahidi na wamemtahadharisha asimwingilie mh. Raisi kiutendaji. Wamesema hawako tayari kwa maandamano yoyote kwani sasa ni KAZI TU.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MWANDISHI UMEANZA VIZURI ILA HAPO CHINI UMEANZA KUTUVURUGA...WE KAMA UNAMPIGIA PROMO MHESHIMIWA KUWA WAZI ACHA MAJUNGU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona hasira?unadhani hizo habari kaziunganisha toka wapi,ni kwenye mitandao na mitaani,ni kweli hali iko hivyo kama huamini baki hivyo ulivyo.lakini HABARI NDIO HIYO.

      Delete
  2. Tatizo UELEWA WAKE NI MDOGO huyo mwandishi na ni MCHOCHEZI, kwa wale wanaokurupuka wanaweza kukurupuka nae LKN kwa waelewa wanajua ANA UFINYU WA KUELEWA MAMBO au mweupe kichwan!

    ReplyDelete
  3. Piiippoooooozzzzzzzzzz PWAAAAAAAAAAAAA

    POWER YOTE TUMEMPA MAGUFULI aka TINGA TINGA, AMETINGA NAYO IKULU

    ReplyDelete
  4. Kiongozi yeyote yule anapochaguliwa na kuanza kazi lazima apite na kutembelea vitengo karibia vya vyote, hii ni protocol hata kwa Kikwete tuliona, miaka mitano si haba tusubiri tuone baada ya mwaka mmoja mtingo ule ule au

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad