Katibu Mkuu Aisikitikia NCCR, Asema Historia itawahukumu...Na Ndicho Kinachowatokea Sasa


Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe amesema kuwa alitabiri kwamba historia itawahukumu na ndicho kilichotokea.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Nyambabe alisema hana jipya la kuzungumza kwa sababu alishazungumza kuhusu mustakabali wa chama chao ndani ya Ukawa, huku akisisitiza namna ambavyo historia itawahukumu.

“Sina la kusema kwa sasa, nilizungumza sana kuhusu kinachoendelea ndani ya Ukawa. Nilisema historia itatuhukumu, niliona mbali, niliyoyazungumza hayajapitwa na wakati,” alisema.

Novemba, mwaka huu viongozi wa chama hicho akiwamo Makamu Mwenyekiti (Bara), Leticia Mosore, katibu mkuu, baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na viongozi wengine walizungumza na waandishi wa habari na kuonyesha shaka ya chama chao kuwa ndani ya Ukawa.

Katika mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Landmark, Dar es Salaam, viongozi hao walitoa tamko kwa kile walichodhani ni anguko la chama chao kuwa ndani ya Umoja huo wa Katiba ya Wananchi.

Akitoa tamko hilo, Mosore alisema kuwa miongoni mwa mambo waliyokubaliana katika umoja huo ni namna ya kujiendesha, ikiwamo kuunda kamati za kutatua matatizo kama Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati ya Ufundi na Kamati ya Wataalamu walizodai zimeshindwa kufanya kazi ipasavyo.

Alisema viongozi hao wameshindwa kuweka kanuni za uendeshaji na kuacha mambo yafanyike kiholela, kamati kushindwa kushughulikia migogoro baina ya vyama, kushindwa kuunda na kusimamia kamati za majimbo na kushindwa kufikia muafaka wa kuachiana majimbo.

Tamko hilo lililenga zaidi kulalamikia ufinyu wa majimbo 12 waliyopewa ikilinganishwa na majimbo 67 waliyosimamisha wagombea mwaka 2010 wakiwa wa kama chama kinachojitegemea.

Mosore pia alilalamikia kuwa licha ya chama chao kurudishwa nyuma, wanahujumiwa kwa sababu bado wanachama wa vyama vingine vilivyo ndani ya umoja huo walikuwa wanang’ang’ania kusimamisha wagombea kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano huo ulionyimwa baraka na chama ngazi ya Taifa, Nyambabe alizitaja kasoro nyingine kuwa ni kushindwa kukubaliana katika baadhi ya mambo aliyodai mwenyekiti wao amekuwa akiyafumbia macho, ikiwamo kushindwa kupata muafaka wa namna ya kuachiana wagombea udiwani.

Suala jingine alilolalamikia ni kushindwa kuonyesha na kukubaliana kila chama kitapata nafasi gani na ngapi iwapo Ukawa ungeshinda na kuunda Serikali, kushindwa kufuata utaratibu wa kumpata mgombea urais wa umoja huo na kuwapa umuhimu mkubwa wanachama kutoka CCM.

Nyambabe pia alilalamikia kutokuwa na timu ya kampeni ya umoja huo ambayo ingewasaidia wagombea wote na Chadema kuwa na nguvu kubwa katika umoja huo ikiwamo kutumia fedha inavyotaka.

Viongozi hao pia walitoa wito wa kumshauri Mwenyekiti wao, James Mbatia aitishe vikao vya kikatiba ili wajadiliane kuhusu hatima ya chama chao.

Mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye ameshindwa aliliambia gazeti hili kuwa hana la kusema juu ya madai hayo kwa sababu siyo msemaji wa chama hicho.

Alisema chama hicho kitakuwa na mkutano na waandishi saa tano asubuhi leo na majibu yote ya mustakabali wa chama yatatolewa.

Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alipopigiwa simu zote mbili zilikuwa zinaitwa bila majibu.

Katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita, chama hicho kilipata jimbo moja tu la ubunge la Vunjo ambalo ameshinda Mbatia. Kabla ya uchaguzi huo kilikuwa na majimbo manne ya Kigoma Kusini, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini na Muhambwe, lakini katika uchaguzi majimbo hayo yamepotea.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha mbwembwe. Ukitaka ubinafsi ndio huu unaouongea. Walichofanya ukawa ni njia pekee kuing'oa CCM. Lakini watu kama nyinyi mliotanguza maslahi binafi mbele bila kuona maslahi ya nchi kwa ujumla matokeo ni haya. Ni CCM ndio waliochakachua kupitia watu kama wewe ambao hawakujifunga buti vipasavyo. Walizzidi kulalamika na kuwapotosha wanachama wengine. Mbatia alielewa hii. Ni wewe bado unalivuta gurudumu nyuma.Hamuwezi kiushinda CCM kama NCCR mageuzi kwa mtazama wangu. Naomba jiendeleze kifikra na uuone umoja uliofanyika hapa. Ni nadra kutokea. Sasa usiwarudishe waliounga mkono kwa sasa. Badala yake kama alivyozungumza Lowassa vita inaanza sasa. Na lazima muwafunde Vijana. Wengi sana waliwaunga mkono sababu walimwamini Lowassa na viongozi wa Ukawa. Waliamini kielimu nchi ingebadilika, kifikra, na kiajira nchi ingefika mbali sana.
    Bado Vijana wengi wenye mwamko na waliosota kujisomesha bila upendeleo waliona Ukawa tegemeo lao. Hili ndilo Taifa la kesho. Napenda kuwapongeza Vijana wote Wa Tanzania, na ninapenda kuwaomba wasikate tamaa, napenda kuwaomba waanze kazi za kuungana leo hii kuelimishana kwamba maslahi yao ni uchi huu unaoibiwa kupitia chama tawala, kwa ndugu zao, Marafiki na makampuni feki na makampuni bepari ya Ulaya, China, Marekani na ughaibuni. Huku ndiko JK alikopeleka mali zenu. Na hawa ndio walio nyuma ya uchaguzi huu kuhakikisha maslahi yao waliyopewa kupitia awamu hii ya Kikwete yanabaki mikononi mwao. Uchaguzi huu ulikuwa ni kukomboa mali asili zetu zinazochukuliwa huku Vijana, Maskini, Wanafunzi kukoseshwa Elimu, ajira, Hospitali bora, Usawa, Uhuru wa kuzungumza na kutenda haki nchini. Tanzania inakuwa kama middle East ambako wageni wachochezi watu wenye maslahi huko ndio chanzo cha Wananchi kupigana wao kwa wao. Watanzania ni watu wa Amani , lakini hawataki kuonewa na kuendeshwa kibeberu. Ni lini na ni Wapi uliona Raisi analeta vifaru kwenye uchaguzi kwa watu wasio na silaha. Ubabe kama huu unaonyesha wazi unyanyasaji wa wananchi na dhuruma iliyotokea. Asiyetaka kushinwa si mshindani. Raisi Kikwete na Viongozi wachache pamoja na Mkapa ndio Wahusika wakuu wa janga hili linaloendelea nchini. Huyu Pombe waliyempachika kama hana Maono na inteligensia kapewa mzigo mkubwa zidi ya uwezo wake. Namuombea afanye na alete haki , umoja, na alete katiba ya wananchi mara moja. Pia Awapeleke watu wa ESCROW kunakohusika. Kama alivyoahidi kukomesha rushwa afanye hivi pia mara moja. Arudishe Imani kwa Wananchi tena. na kama anawaona marasi waliopita wanamakosa asimamie haki za Wananchi.
    AMANI HAKI, UKWELI,Umoja, Uadilifu uboreshwe Tanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mabadiliko tunahitaji lakini sio kwa lowasa tafuteni mtu wa upinzani wa kugombea acheni ushabi mbuzi sumaye alikua madarakani miaka kumi akiwa mtendaji mkuu leo anatudanganya wazi kua ccm wameharibu nchi wakati wana haribu yeye alikua wapi? lowasa yeye alikua wpi acheni ushabi tume choka na ccm lakio sio mnavotaka kutupeleka wapo watu nyuma wanao natakula kuptia mgongo wa lowasa acheni kupumbaza watu penye ukweli ongeeni ukweli lowasa hawezi kukuletea mabadiliko umeshindwa kujiletea wewe kaa kmya tafuteni mtu mwingine wa kusimama tutamchagua acheni kutudanganya sisi sio watoto tunajielewa hatuwezi kudumbukiza taifa kwenye shimo msubirie ukawa wenu kusambaratika maana mboe ameuza haki waaakulaumiwa ni mboe wala sio ccm pesa kitu kibaya sana leo mnasimama mnalaumu nini nanani mnae mlaumu mboe ndio wakulaumiwa chama kilichoaminiwa leo kika thamini pesa kuliko nchi umoja sio mbaya wabaya mlio waweka kubeba dhamana ya nchi kwa hiyo kaeni kimya msilalamike kwenye kampeni za ukawa hapakua hata na suala la ufisadi badala yake ccm ndo wakawa kinara wakuzungumzia hafu bado mlitaka tuwachague tunaanzia wapi? acheni ushabiki mbuzi

      Delete
  2. KELELEEEEEEEEE NI UJUNGA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad