Katika hali isiyo kuwa ya kawaida Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Shinyanga leo kimedai kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo limefanya maandamano ya Chadema bila kujijua.
Kwa mujibu wa baadhi ya viongozi wa chama hicho walidai kupokea taarifa kutoka kwa uongozi wa juu wa chama hicho ukiwataka kufanya maandamano leo nchi nzima ya kupinga ushindi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa madai kuwa demokrasia imebakwa katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 oktoba 2015.
Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama amesema kwamba chama hicho kimefanikiwa kufanya maandamano kupitia jeshi la polisi lililozunguka mji mzima kuwasaka wanachama wa chadema na kuambulia patupu.
“Tulipanga kufanya maandamano leo Novemba 03,2015 mji mzima wa Shinyanga lakini polisi ndiyo wamejitokeza kufanya maandamano wakiwa na magari yao kila mtaa.”Alisema Kitalama.
Kufuatia taarifa ya Chadema kutaka kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini Askari wa Jeshi la Polisi wamekuwa katika misururu ya magari yakiwemo ya maji ya kuwasha wakizunguka kuwasaka waandamanaji kutoka chama hicho ambao hawakufanikiwa kufanya maandamano hayo.
Jijini Dares salaam Askari Polisi wakiwa kwenye punda na wengine wa doria wameonekana katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo nyeti na yenye ofisi nyingi za Serikali ikiwemo Posta.
Tukisema CHADEMA mna matatizo ni halali kabisa,hayo nayo kwa mtu mwenye akili timamu angejitapa hivyo?kwani polisi si wako kazini?yaani sijui mmelishwa nini nyie wenzetu.Mungu awasamehe kwa yote.
ReplyDeleteAmakweli chadema mbumbumbu, eti wanajisifia kama machizi....piiiipoooozz PWAAAAAA!! Power yote wamempa Magufuli anaenda nayo magogoni
ReplyDeleteInatia huruma kama kiongozi wa chama kwa ngazi ya wilaya anaongea upuuzi kama huo kweli Chadema kuna walio timamu?? Ni chama cha wavuta bangi hicho na ni bora tutafute mbinu ya kukiua kabisa la sivyo tutakuja tawaliwa na viongozi wavuta bangi.
ReplyDeleteUPUMBAVU NDIO UNAO WASUMBUA
ReplyDeleteNa ujinga wenu CCM na serikali yenu
ReplyDelete