Saa chache baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Magufuli ameanza kazi kwa kasi zaidi ambap leo hii ameanza kazi kwa kumteua mwanasharia mkuu na kuitisha bunge.
Akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya serikali katika viwanja vya Ikulu Jijijini Dar es salaam katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Rais Magufuli amaenza kazi leo hii kwa kumteua mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ni George Mcheche Masaju aliyewahi kushikilia nyadhifa hiyo, katika serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwanasheria huyo mteule anatarajia kuapishwa kesho saa nne asubuhi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali
Aidha Balozi sefue ameeleza kuwa Rais Magufuli ameitisha Bunge la 11 ambalo litafunguliwa rasmi tarehe 17/11/2015 nakuongeza kuwa huenda mpaka kufikia tarehe 19 mwezi huu Rais atakuwa amependekeza jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu ya tano na kusubiri ridhaa ya wabunge.
Kazi Imeanza: Rais Magufuli Amteua George Masaju Kuwa Mwana Sheria Mkuu wa Serikali
2
November 05, 2015
Tags
Mtu WA watu huyu
ReplyDeleteKabila gani huyu
ReplyDelete