KIAPO: Kassim Majaliwa Aapishwa Rasmi Ikulu Ndogo Dodoma Kuwa Waziri Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, asubuhi hii amemuapisha Mbunge wa Ruangwa, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mjini Dodoma.


Hafla ya Kumuapisha Mh. Majaliwa imefanyika kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. samia Hassan Suluhu, Rais wa Zanziba, Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais Msitaafu, Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Wabunge, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Wabunge na wageni wengine.

KIAPO CHA WAZIRI MKUU - NOV.20.2015| TBC

Mh.Kassim Majaliwa akila kiapo cha utumishi na baada ya hapo amekabidhiwa katiba ya nchi na Rais Magufuli kama nguzo au muongozo katika kazi zake.

Posted by Simu.TV on Friday, November 20, 2015
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. chamwino imekuwa ikulu ndogo HAIPANDI CHEO kwa miaka 44 sasa,na bado inaitwa ikulu ndogo.baada ya shughuli hii magufuli anarudi dar kwenye bahari na mengineyo.magufuli alisema yeye ni mabadiriko ya kweli,lakini tunapoziona dalili tunasema wananchi hatuwaelewi ccm.wale wale,yale yale.changa la macho.

    ReplyDelete
    Replies
    1. pumbavu ww tafuta pengine pa kusimamia

      Delete
  2. siielewi hii picha naona watu lundo wanaapa wangapi ,na wanaapishwa wangapi pawe na utaratibu mzuri,haipendezi.anayeapisha na anayeapa full -stop.ondoeni aibu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad