Kubenea Aibua Ufisadi wa Billion 1.2 Kupitia Ufuaji wa Majoho ya Madiwani

MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ameibua ufisadi wa Shilingi bil. 1.2 kwa mwaka katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam unaofanywa kupitia ufuaji wa majoho ya madiwani.

Kubenea amesema hayo Stendi Kuu ya mabasi yaendayo mikoani alipofanya ziara ya siku moja kutembelea soko la Urafiki maarufu kama Mahakama ya ndizi, soko la Mabibo na kuhitimisha ziara yake katika Stendi za Ubungo na Simu 2000

“Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa mradi huo wa ufuaji majoho kabla ya madiwani kufanya kikao unaotumia shilingi bilioni 1.2 hivyo basi Halmashauri ya Manispaa itakayokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tukianza kazi tutaufuta,” alisema Kubenea.

Aliongeza kuwa kufutwa kwa mradi huo kutafanywa mara moja baada ya Ukawa kupata Meya wa Manispaa na Jiji kutokana na ukweli kwamba wana Halmashauri mbili kati ya tatu hivyo zitawawezesha kumpata Naibu Meya katika Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kubenea alisema jambo jingine ambalo watakalolisimamia ni kuhakikisha wanaondoa Mahakama ya jiji kwa sababu wamegundua hakuna mahali popote katika bara la Afrika.

“Mahakama hiyo ni ya kikoloni kwani hakuna mahali popote katika bara la Afrika ambako ipo zaidi ya Tanzania kwenye jiji la Dar es Salaam, hivyo ili kuwaokoa mama lishe, madereva bodaboda, machinga ni lazima tuhakikishe Mahakama hiyo tunaifuta,” alisema Kubenea.

Mbunge huyo alisema wamedhamiria kwenda kufuta zuio madereva wa bodaboda kuingia mjini lililokuwa limewekwa chini ya aliyekuwa Meya wa jiji, Dk. Didas Masaburi ili kuwawezesha vijana hao kufikia katika mji huo.
Chanzo: Magazetini
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kubenea sasa unaanza kuchemsha,iko hivi meya atoke CCM au UKAWA haijalishi,nyie sasa muwe kitu kimoja.NI KAZI TU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. CCM washakula vya kutosha wacha wengine wafanye kazi ww vp????????alaaaaa

      Delete
    2. mazaburi meya kala mnooooooo ona mtumbo ule na miziwa.

      Delete
  2. HEKO MHESHIMIWA KUBENEA.NI WAZI UKAWA MTAKAPOLIKAMATA JIJI MTAYAGUNDUA MADHAIFU KIBAO,WIZI,ULAGHAI NA KIMOJA MKIJUE,MADIWANI WACHACHE WA CCM MTAKAOKUA NAO WATAWACHIMBENI SANA,WAMEZOEA WIZI NA UHUJUMU TUNAJIANDAA KUWA-FLUSH OUT CCM WOTE 2020

    ReplyDelete
  3. kazi moja kivipi washirikiane kuendelea kupiga hela za wananchi.

    Ama kweli ukistaajabu ya Musa.

    ReplyDelete
  4. Mnaboa bana,Mafisadi wako ukawa,na wako ccm.Sema
    tuanze Tanzania mpya.

    ReplyDelete
  5. Msitake kufanya vitu kwa kukomoana lini bodaboda ikawa ajira au chombo cha usafiri, mshughulikie vijana kuwapatia ajira, elimu za kujitegemea au mitaji ya kujifanyia shughuli za uhakika. Kuna nchi gani umeona bodaboda zinatumika kama chombo cha usafiri katikati ya mji. Mnataka kuanza kuteletea ujambazi na watu kumwagiana tindi kali.Bodaboda si chombo cha usafiri.

    ReplyDelete
  6. Eti aibua ufisadi......gazeti lake lilimwandika sana Lowasa kama ni fisadi, mpaka akam-mwagia tindikali, Kubenea huyo-huyo akashiriki kumpigia debe Lowasa ETI awe rais wa TZ - maajabu ya karne!!!.........ni UNAFIKI ndio unaokusumbua Kubenea, we'mwenyewe KIBAKA tu........UNGEANZA NA LOWASA..........hebu msituchoshe, mkiona hamtajwi-tajwi basi mtazua la kuzua ili msikike .........hovyoooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad