Kuhusu Emmanuel Nchimbi: Kama Hatakiwi kuwa Spika, kwanini Alipewa Fomu?

Ifike mahali CCM, kama chama chetu na chama tawala, kijitenge na siasa za ulaghai, uongo na maigizo. Hasa kwenye mambo nyeti ya nafasi za kiuongozi. Tangu Emmanuel Nchimbi alipochukua fomu ya kugombea Uspika wa Bunge la 11, amekuwa gumzo kwa viongozi na wanachama wa CCM. Kuanzia Makao Makuu ya CCM hapa Dodoma hadi Ofisi Ndogo za Lumumba Dar es Salaam, Nchimbi anasemwa kama asiyefaa na kibaraka.

Anakandiwa na kusingiziwa kuwa bado ni mfuasi wa Lowassa pamoja na kushiriki kampeni za Rais Magufuli. Nchimbi anafanyiwa na kusemewa vitimbi. Yote haya ni kuonesha kuwa Emmanuel Nchimbi hatakiwi kuwa Spika. Kwanini alipewa fomu ya kugombea? Hivi bado CCM yetu inategemea 'vijihela' vinavyotokana na kutoa fomu za kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama?

CCM ikumbuke kuwa Dr. Kalokola, yule aliyedai milioni moja yake ya fomu ya Urais, amechukua tena fomu ya Uspika. Huyu aweza kuungana na watu aina ya akina Nchimbi kudai hela yao ya fomu za Uspika. Itakuwa aibu kwa CCM zaidi kuliko kwa wagombea husika. Chama kitaonekana ni cha kitapeli,kilaghai na kimaigizo. Waliochukua fomu za Uspika waachwe wapambane kichama na mmoja wao awe mgombea wetu wa Uspika. Majungu hayajengi chama!

By Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CDM mmeanza hujuma zenu na fitina haiwahusu hata kidogo huo usipika kwani mmeanza kujenga kambi za Lowassa ndani ya CCM ili watu wajue kwamba Nchimbi kaonewa kisa Lowassa la Spika hilo ni swala la CCM kumchagua yeyote atakae wafaa sio nyie CDM mnachukulia kama vile ni furusa ya kuivuruga CCM MTASOMA SANA NAMBA MWAKA HUU MPAKA 2020 MTAKUFA NA KIHORO

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe pimbi kweli, sasa Chadema hapa wanahusika vipi? mmeshaanza changanyikiwa eehhh?

      Delete
    2. Weye ndo pimbi waachieni ya Nchimbi na CCM sio kutuletea mada za kishabiki tolea mbali uchaguzi umekwisha kampeni za nini za kuchambuana

      Delete
    3. nenda shule ukasome wewe pimbi uelewe jinsi ya kuitafakari habari!! manake naona hapo elimu niduni! hovyooo kabisa, iongelewe habari ya ccm, wewe uwaingize Chadema! unajielewa kweli wewe!

      Delete
  2. Hivi ukimfumani mkeo na Juma,mkasuluhisha na kuombana msamaha na maisha yakaendelea baada ya hapo,hata kama atakuwa anakupikia,kukufulia n.k utakuwa na imani nae kiasi kwamba siku ukija kumuona yuko na Juma tena usijiulize maswali kichwani mwako?Nadhani hii ndio inawasumbua CCM,tatizo ni kwamba kwa nini walimpa form,na kwa nini wasimuambie ukweli.

    ReplyDelete
  3. Sitta huyu na vijana wake mtu mzima ovyo

    ReplyDelete
  4. Ndani ya ccm Lowassa yupo kila kona.Wabunge wa Lowassa kibao,kwenye Kamati kuu,Halmashauri ku,Wajumbe wa Mkutano mkuu.Ni hivi mnamkataa nchimbi lakini mjue kauli ya mwisho ya nani awe spika itatoka kwa Lowassa na sio kwa Magufuli.nguvu ya CHADEMA kwa sasa ipo kila upande kila kona.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad