Lowassa Abadili Msimamo Wake wa Kwenda Kuchunga Ng'ombe Asema 'Nimepoteza Pambano Siyo Vita'

Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amesema ataendelea kushiriki kikamilifu katika siasa na kubainisha kuwa utaendeleza mapambano ya mabadiliko kwa kudai Katiba Mpya.

Lowassa aliwaambia wanahabari leo kuwa kasi ya ufanyaji wa siasa itaongezeka kuliko ilivyokuwa awali na kwamba kwa sasa anaweza akawa “amepoteza pambano lakini siyo vita.”

Kauli hiyo ya Lowassa inabadilisha msimamo wake wa awali aliokuwa wameutangaza kupitia mahojiano na Shirila la Habari la Uingereza (BBC) kuwa iwapo angeshindwa kinyang’anyiro hicho cha urais angeenda kuchunga ng’ombe kijijini kwake Monduli mkoani Arusha.

Mwanasiasa huyo, ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani, alisema Ukawa itaendelea kudai Katiba Mpya ya wananchi itakayohakikisha kuwa Tanzania inakuwa na tume huru ya uchaguzi na serikali inayowajibika kwa umma.

Ni wazi kuwa uchaguzi mwingine katika mazingira ya sasa na chini ya katiba ya sasa hauwezi kuzaa matunda tofauti. Bila katiba mpya ya wananchi, Tanzania haitakuwa na demokrasia na itaendelea kuwa nchi  inayotawaliwa kwa mizengwe na udikteta wa CCM,” alisema Lowassa.




Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. We Lowassa uko mwongo na ndio maana hukushind uchaguz. Nani atakae kuaminia na hayo usemay? ulisha zeeka acha nend upumzik hata ujichagulish marangap hutaingiag ikulu. Ushaur wang kwak ni kutulia na familia na marafik na kusaidia serekal kwa ushaur sio kulazimish ikulu na utajisababishia matatiz ya moyo ukingangania kuingia ikulu. Pamekukataa. Eti utachung ngomb ukishindw haya kazichung sasa? achen kudangany wanainch na manen ya uongo na hiyi inadhihirish kwamb hata ungeshind hung timiz yal ulikua umeahid watanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwendraa sema wewe siyo watz (sisi tuliowengi tunamkubali saaana).

      Delete
  2. Umetamka mwenyewe kwa kinywa chako ukishindwa utaenda chunga ng'ombe kulikoni tena? ? Jamani hivi kwa umri huo ulionao bado unataka after 5 year's ushindane tena?? Free advice mzee nenda kapumzike wacha siasa sasa. .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uwiiiiii umeua!kuna kiongozi mmoja alitamka kuwa vyama pinzani sio rahisi kukubali kushindwa kihalali,wao siku zote kilio chao ni kuibiwa kura,wana mbinu nyingi za kushawishi watu wakubali kuwa wameibiwa kura,na kwamba alishangaa kusikia Lowasa akishindwa ataenda kuchunga ngo'mbe.Ukweli ni kwamba ukiona mfanya biashara mkubwa anang'ang'ania urais ujue kuna kitu anatafuta,hasahasa ukwepwaji kulipa kodi kihalali,na kama Lowasa angeshinda kungekuwa na tofauti kubwa sana kati ya maskini na matajiri.Tumshukuru Mungu kwa kutuepushia hilo.

      Delete
    2. kwani mnamuogopa eee!! mbona pressure zimewapanda sana jamani!!

      Delete
  3. Nadhani lowasa ulipokuwa ccm wewe ndio ulikuwa mpinzani mkubwa wa katiba mpya leo umeweka.miba kwa njia unayopita mwenyewe ni ngumi watu kukuamini

    ReplyDelete
  4. Mzee unajidhalilisha, unachohangaikia nini, mabadiliko waachie vijana, si kwa kuchoka huko

    ReplyDelete
  5. Ipo siku watakuelewa tu.Mungu akusimamie Mh Lowasa

    ReplyDelete
  6. WATANZANIA HATUHITAJI VIONGOZI WAONGO, WEZI, MAFISADI PAPA WALA VIGEU-GEU KAMA LOWASA, KWANZA ALISEMA ANAHITAJI KURA 10M ASHINDE, BAADAE AKASEMA KAPIGENI KURA ULINZI NIACHIENI MIMI, MARA MKISHAPIGA KURA LINDENI KURA ZENU, GHAFLA NIMEIBIWA KURA NILIPATA KURA M10, KUBWA KULIKO NIKISHINDWA NITAENDA KUCHUNGA NG'OMBE, YAMEGAUKA TENA 'BADO NATAFUTA' ........................!!!!!????!!!!

    ReplyDelete
  7. Sipati picha kama rais angekuwa Lowasa,mmmmmh jamani Mungu kajua nini ingetokea ndio maana katuepusha na balaa la UKAWA kushika nchi chini ya Lowasa.Asante Mungu!HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  8. hakuna jipya lolote tanzania

    ReplyDelete
  9. LOWASA NI FASIDI TU HANA LOLOTE ALIKUWA WAZIRI MKUU KAIBA PESA

    NA SASA ANAJIFANYA MJUAJI NAIMANI SI MUDA MREFEFU ATABURUZWA KWENYE

    MAHAKAMA YA MAFASIDI NA NDIO ITAKUWA MWISHO WA LOWASA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad