Lowassa Alivyoipaisha CHADEMA Katika Uchaguzi Huu, Ni Asset na Ataendelea Kuwa Asset

LOWASSA ni "Asset au Liability.

-Kabla ya ujio wa Lowassa ndani ya chadema, chadema ilikuwa na majimbo 23 tu na viti maalumu 26 na kuwa na wabunge 49 ktk bunge la 10 la 2010-2015, ujio wa Lowassa umeongeza wabunge kutoka majimbo 23 mwaka 2010 hadi majimbo 35 mwaka 2015 na viti maalumu kutoka 26 hadi 43 na kufanya jumla ya wabunge wa chadema 78 ktk bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na chama cha upinzani tangu Tanzania ipate uhuru, Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"

-Kabla kuondoka kwa Lowassa ndani ya ccm, ccm ilikuwa na wabunge wa viti maalumu 79 mwaka 2010, sasa ccm itakuwa viti maalumu 62 tu kwa maana hiyo nguvu ya Lowassa imeondoka na viti maalum 17 ambao wote imebidi wapewe chadema, na ndiyo maana sasa chadema itakuwa na viti maalumu 43, which means, chukua viti 26 vya cdm 2010 + viti 17 alivyokuja navyo Lowassa = 43, Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"

-Mwaka 2010-2015, ccm ilikuwa inapokea ruzuku zaidi ya 78% ya ruzuku yote ya vyama vya siasa kutokana na kura za urais alizopata JK, mwaka huu ccm itapokea ruzuku isiyozidi 59% ya ruzuku yote ya vyama ni sawa pungufu ya 20% waliyopoteza ccm, Na kwa mara ya kwanza chama cha upinzani chadema kitapokea 40% ya ruzuku yote ya vya siasa, hii ni kutokana na kura mil 6=39% alizopata Mhe. Lowassa. Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"

-Kabla ya ujio wa Lowassa, katika majiji matano (5), Mbeya, Dar, Tanga, Mwanza & Arusha, cdm ilikuwa haiongozi hata jiji moja kati ya hayo kwa mwaka 2010-2015, yote yalikuwa chini ya ccm, Ujio wa Lowassa umeifanya chadema kuongoza majiji 4 (Mbeya, Dar, Arusha & Tanga japo Tanga itakuwa chini ya UKAWA) kutokana na ushindi wa madiwani wake ktk majiji hayo na ccm imebaki na jiji la Mwanza pekee, which means ccm imepoteza majiji 4 kutokana na kuondoka kwa Lowassa. Je Lowasa ni "Asset" au "Liability"


-Mwaka 2010-2015 chadema ilikuwa inaongoza halimashauri 5 nchi nzima mfano: Moshi & Karatu, mwaka 2015 kwa mara ya kwanza chadema itakuwa inaongoza halimashauri 30 Tanzania hii ni kutokana na Ushindi wa madiwani na wabunge ktk halimashauri husika. Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"



NB: Kwa mtu wa kawaida na anayefikiria ya leo bila kujua kesho itakuwaje alibeza ujio wa Lowassa ndani ya chadema, lakini kwa anayefikiria leo na kesho na kuangalia kwa jicho la tatu atakuwa amegundua umuhimu wa ujio wa Mhe. EDWARD LOWASSA.

Ahsante...!!!

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. he is an ASSET big time!!! wengi uraisi tulikuwa 50 50, lakini tulitaka wabunge wa upenzani waongezeke bungeni!! safi saanaaa ENL, bado tupo nyuma yako.

    ReplyDelete
  2. Dr. Slaa upo???? Hii inaonesha kua yeye Dr. Slaa ndio alikua liability kwa kua hakuna kilichopungua kwa kujitoa kwake chadema.

    ReplyDelete
  3. Dr silaha miaka 100 watanzania kumpa kura lowasa ni kwamba waliichoka ccm,,, ila hawakuelewa kuwa Lowasa ni ccm no 2,,,, aliyevaa kivuli cha ukawa,,,, Mabadiliko mngeyapata kwa Dr Slaa,,, alikua hana kashfa, ,, ila lowasa Fisadi Papaa, please acheni siasa za maji taka kumpenda mtu kisa asira ya chama,,,, mbona wameshindwa kutaja kashfa ya Magufuli,,, acheni jembe lifanye kazi yake,,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umenena mwanangu!! Heshima kwako!

      Delete
    2. Senge wewe funga domo lake na kura za wizi
      Watanzania rais wetu Lowassa tu ktk mioyo yetu

      Delete
  4. Mimi nina amini kila mmoja ana mchango Lowasa na Slaa. Lowasa amekuta taasisi imejengwa na Slaa, lakini nae amekuwa na mvuto wake, kama angeenda ACT asingeleta mafanikio maana hakijajingenga vizuri

    ReplyDelete
  5. matusi ya nn www unaetukana....toa hoja za msingi...wenzako wametoa hoja zilizoenda shule..tatizo vijana wa kitanzania mnakurupuka no reason behind,no research at @ll...ndomana atuelewi tunazidi kuwa wajinga kimantiki...unaleta ushabiki lowasa lowasa...heat to the point matusi ya nn/ata familia yako utaiongoza kwa kuitukana una akili...that is my desicion we unaetukana...full stop.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad