Maalim Seif azugumza na Balozi wa EU na viongozi wa UKAWA....Atoa Msimamo Mzito

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea kauli yake ya kutotambua kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao cha mashauriano na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Maalim Seif amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bw Jecha Salim Jecha hana mamlaka ya kufuta uchaguzi huo, na kinachohitajika na kuendelea na mchakato wa kuhakiki kura zilizobakia na mshindi kutangazwa.

Kuhusu tamko lililotolewa na serikali juu ya kufutwa rasmi kwa uchaguzi huo kupitia tangazo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali tarehe sita mwezi huu, Maalim Seif amesema tamko hilo limekosa uhalali tangu lilipotolewa na Mwenyekiti wa ZEC.

Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF amesema Chama chake hakijalizingatia tamko hilo na wala hakijadili uwezekano wa kurejewa kwa uchaguzi huo, kwa madai kuwa uchaguzi ulikamilika bila ya kuwepo malalamiko kutoka chama chochote cha siasa na wala Tume ya Uchaguzi.

Mapema akizungumza baada ya kikao hicho cha mashauriano, aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa amesema kikao hicho kilichojadili Mkwamo wa kisiasa Zanzibar kimekwenda vizuri.

Hata hivyo amesema ufafanuzi zaidi utatolewa Jumapili ijayo ambapo viongozi hao wanakusudia kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kikao hicho Maalim Seif alifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Filberto Seregondi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuelezea hatua zinazochukuliwa kukwamua mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Balozi Seregondi ambaye anamaliza muda wake wa utumishi hapa nchini,aliambatana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Tanzania kutoka Umoja huo.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi nashangaa kwa nini kajitangaz mshind ? huyo Seif kwanz afungulie mashitaka ya kukiuk katib na sheria. Kwan naon alitak vurug ndio maana kajitangaz mapem kwan ninjam walifany mapem ili ajitangaz mshind wakikataa basi vurug zianz. Kwahiy akun alie juu ya sheria ns anae vunj sheria hufikishw mbel ya vyomb vya usalam na kufunguliwa mashtak sasa Seif na yeye afungulie mashtak.

    ReplyDelete
  2. Mpumbavu mkubwa we kwani kujitangazia ushindi ndiyo uchukuliwe sheria matokeo yalikuwa yameshabandikwa na mwanasheria mkuu fatma karume kasema ss tatizo nn ww ukifanya mtihani matokeo huwekwa si unajua km umefaulu au huku faulu tatizo liko wapi km sefu kajitangazia mlizowea kuiba safari hii mkono wamungu umewaumbua zanzibar mtaitowa mkitaka msitaki sio kisiwa chenu mfanye mtakalo pl muwapishe na vyama vyengine tuwaone waroho wa madaraka nyiye kz kulazimisha tu wala hakuna anowataka

    ReplyDelete
  3. Afunguwe mashtaka ya nn na kashinda ukweli mlizowea kuiba safari hii mmeumbuka lini kashindwa sefu pl zanzibar si mnaiba kura tu mnandikisha hata wafu mnaleta mijitu kutoka bara kupiga kura mikutano yenu mnaungaunga tu hmna anayoipenda ccm ww unaipenda unafaidika ss maskini tunafaidika nn

    ReplyDelete
  4. acha upumbavu wewe, si umshtaki wewe kwani sheria imekuzuwia, watu wengine bhana hamjielewi hata kidogo, km anavunja amani hata ww unahaki kumshtaki usisubiri mtu au umezoweshwa kufanyia bwabwa wewe huwezi kujisimamia, mambo msojua nyamazeni msioneshe ufala wenu ktk jamii

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad