Rais John Magufuli amelaani vikali kitendo cha Wabunge wa Vyama vya Upinzani kuzomea leo bungeni.
Rais Magufuli ameeleza kuwa tabia iliyofanywa na wabunge hao inaonesha jinsi ambavyo hawajakomaa kisiasa na kuwaita watoto huku akimpongeza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa kuendelea kubaki Bungeni.
“Ndio maana nimempongeza sana Mheshimiwa Zitto. Mheshimiwa zitto umekomaa na naamini hata wana CCM kule Kigoma walikuchagua,” alisema rais Magufuli.
“Mmeona tuna kazi kubwa, bado tuna watoto wengi. Tuendelee kuwavumilia, nadhani na watanzania wameona,” aliongeza.
Aliwataka wabunge wote kusimama pamoja bila kujali itikadi zao za vyama na kuwasisitiza kuwa wanapaswa kuhakikisha kuwa Bunge la 11 linakuwa bunge la kihistoria na kuacha masuala ya kupigana vijembe, kuzomeana na kutoka nje.
Kwa upande wake Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai alimuomba radhi rais Magufuli na Shein kwa kile kilichoanywa na wabunge wa Ukawa huku akiahidi kuwa hali hiyo haitajirudia tena.
Ndugai aliwaonya wabunge kuwa kitendo kilichofanywa ni cha aibu hivyo hatawavumilia tena na kwamba wabunge wanaweza kumfanya akawa Spika mpole ama kumfanya awe Spika ‘mbabe’.
“Mnaweza kunifanya nikawa Spika mbabe sana… leo iwe mwisho. Ni kwa sababu wazee hawa walikuwepo. Lakini wazee hao wasipokuwepo, wakifanya tena tabia hii, basi… nisiseme sana,” alisema.
Magufuli Awaita UKAWA ‘Watoto’.....Spika Awapa Onyo Kali, Asema Atakuwa ‘Mbabe’ Kama Watarudia Tena
7
November 21, 2015
Tags
wewe ndio mtoto jk kakuuzia kesi umeshindwa kuitatua, unataka kuburuza watu unadhani wote wajinga kama zito ambaye yupo huku na huku, ajitambui,,, kwa hiyo we unaona ni sahihi kutokutangazwa rais wa zenji mpaka leo halafu unaita wenzio watoto. jiheshimu ili hueshimiwe.
ReplyDeleteTutaona karibuni wewe na UKAWA nani mtoto, hii nchi yetu sote tusitukanane wala kudharauliana kwasababu ya nguvu za dola
ReplyDeleteWEWE ULIOANDIKA HAPO JUU UNAONEKANA MLALA HOI KWANZA NENDA KAJIFUNZE
ReplyDeleteKWA WATOT
W EWE NDIO MTOTO ULIYO ANDIKA HAPO JUU KWANZA UJIHESHIMU SANA
ReplyDeleteWEWW NDIO MJINGA SANA
ReplyDeleteKWELI UKAWA NI WATOTO, WAKIKUA WATAACHA
ReplyDeletesaa kama sio utoto nini huo ni utoto tena bora hata mtoto hawezi fanya vitu kama ukawa wanavofanya maana mtoto mwenyewe melewa....vifungu wamesomewa vinajieleza rais wa zanzibar haja apishwa aliowadanganya kuwa suluhisho huwalinatafutwa kwakufanya fujo ninani..mlaumuni lowasa katiba mpya iliyo kuwa inapendekezwa lowasa alikuwa wa kwanza kuipinga alimjibu mzee warioba alipo leta katiba iliyo pendekezwa na wananchi Lowasa akamwambia Warioba katiba yako ulioileta sio sahihi na wala haija toka kwa wananchi leo mnamlalamikia nani acha lowasa aone uchungu ili apate akili mkuki kwa nguruwe kwa binadam mchungu alisha jiwekea asilimia kuwa watakabidhiana nchi na rafiki yake JK sasa kanyea debe akakumbuka na katiba nendeni mkampigie kelele lowasa hapo nitawaona wa maana mkuki kwa nguruwe hahahaha walipotoka kwa rais alishindwa kuhutubia
ReplyDelete