HALI isiyokuwa ya kawaida Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limekiuka sheria na kuanza kupiga mabomu ya macho katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), kuwatawanya wafuasi wa Chadema. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Tukio hilo limetokeaza leo jioni, baada ya wafuasi hao kuanza mvutano na askari Polisi mmoja na ndipo vurugu zilizodumu kwa saa moja na nusu.
Hata hivyo wafuasi hao kabla ya kuanza vurugu hizo, walizima kuruka kuta za hospitali na kufungua geti kwa mabavu.
MwanaHALISI Online ilishuhudia Polisi huyo na wafuasi wa Chadema wakivutana nje ya mlango wa vyumba vya kuhifadhi maiti.
Baada ya mvutano huo wafuasi hao wa Chadema walianza kumuangushia kichapo askari huyo ambaye anatuhumiwa kufanya njama za kurudisha mwili wa marehemu mkoani Geita kwa madai kwamba tukio lilitokea huko.
Hali hiyo ya askari kuangushiwa kichapo, lilikuja gari la polisi ambalo lilikuwa na polisi ambao walikuwa na mabomu ya machozi na silaha za moto na kuanza kipiga mabomu.
Aidha Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia Polisi mmoja akimpiga mjane wa marehemu, katika vurugu hizo ambazo zilianzishwa na polisi wenyewe ambao walilazimisha kuingia kwenye chumba hicho.
Katika vurugu hizo, polisi walimtia mbaroni Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Pastrobas Katambi na baadhi ya wafuasi zaidi ya wanne.
Awali wakati wafuasi wa Chadema wakiupokea mwili wa marehemu, walikuwa walisikika wakiimba, “Kama sio wewe Mkapa na mauaji yangetoka wapi.”
Hata hivyo wafuasi hao ambao waliupokea mwili wa marehemu katika kivuko cha Busisi ambapo walipofika kati kati ya Jiji la mwanza walitokea wafuasi wengine ambao walikuwa nao walisikika wakiimba,” CCM wameua CCM wameua… Hadi katika BMC.
Kifo cha Mawazo kinahusishwa na mmoja wa viongozi wakubwa wa CCM Mkoa wa Geita, ambaye ni mmiliki wa mabasi yanayofanya safari zake Mwanza – Geita.
Kuhusishwa kwa kigogo huyo wa CCM na kifo hicho, inadaiwa kuwa gari lake lilionekana likiwabeba vijana wanaotajwa kuhusika na mauaji hayo na kuwaleta mjini hapa.
Pia kigogo huyo ambaye ni Mbunge mteule wa kati ya majimbo ya mkoa huo, anahusishwa kuandaa mtandao wa wauaji hao ambao mmoja wao anadaiwa kutoka jijini hapa.
Pia Mawazo ambaye alikuwa ni mgombea ugunge jimbo la Busanda akichukuana na Lolencia Bukwimba (CCM) inadaiwa alikuwa anatarajiwa kwenda mahakamani kupinga ushindi wa Bukwimba.
Hata hivyo inaelezwa kuwa endapo kama marehemu angefungua mashtaka polisi angeshinda kesi kutokana na ushahidi wa video zinazowaonesha polisi kuwatisha mawakala wa Chadema kusaini matokeo kwa lazima.
Akizungumza na wafuasi wa Chadema, Godbless Lema, amesema kifo cha Mawazo ni mpango wa Chama cha Mapinduzi na kuitaka Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaohusishwa na kifo hicho.
Source:Mwanahalisi
Ee Mwenyezi Mungu ututetee sisi tulio wengi toka mikono ya wachache wanaotumia dola na vyeo walivyonavyo kutukandamiza na kutuulia wenzetu walioamua kusimama kwa niaba yetu tulio wengi. Wamulike hata wale wanaotumia vibaya MADARAKA na HASA WALE WALIOPEWA MADARAKA na wachache wenye nguvu uwape macho ya rohoni ili watambue kuwa TANZANIA SI MALI YA MTU AU KIKUNDI CHA WATU WACHACHE ILA NI YA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI JINSIA, KABILA WALA DINI. Ee Mwenyezi Mungu usikie kuomba kwetu
ReplyDeletegazeti mwanahalisi na chama ni mwachadema wote haohao
ReplyDeletenionavyo mimi hii nchi ni ya chama kimoja, ningewashauri hao ukawa wakubali kuwaachia kila kitu ccm waendelee kutawala wanavyotaka kuliko hali ya uonevu wanayokabiliana nao mara wanachomwa visu mara mapanga bado kupigwa mabomu mara kuporwa ushindi kule zanzibar hamuoni kuwa mnajiangaisha bila mafanikio.jitoeni wabaki kuuana wenyewe acheni kujitesa hao wenzenu wamejiimarisha kidikteta. jinasueni kwenye mwamvuli wa vyama vingi hiki ni kichwa cha mwendawazimu.
ReplyDelete