Marekani Yaipa Kibano Tanzania .....Yaitaka Serikali itoe Maelezo Uchaguzi Zanzibar na Sheria ya Mtandao , Yatishia kusitisha Msaada wa Trilioni

Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) wa Marekani umeonya kuwa hali ya kisiasa Zanzibar na tukio la hivi karibuni la watu kukamatwa chini ya sheria mpya ya uhalifu mtandaoni yanaweza kuathiri vigezo vya kuiwezesha Tanzania kupata msaada.

Katika barua ya MCC ya Novemba 19, ambayo imesainiwa na Naibu Makamu wa Rais wa Idara ya Operesheni ya Miradi kwa Afrika, Jonathan O. Bloom kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, mfuko huo umetaka maelezo kuhusu utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar pamoja na ufafanuzi wa sheria ya uhalifu wa mtandaoni.

“MCC inashukuru kwa uongozi na dhamira yako wakati wa mchakato mzima wa maendeleo ya mradi huu. Msaada wa dola milioni 472 (ambazo ni zaidi ya Sh trilioni moja), una nafasi kubwa ya kusaidia kuleta mageuzi katika sekta ya nishati na kuwaunganisha maelfu ya watu katika gridi.

“Lakini mgogoro wa Zanzibar na ukamataji watu wa hivi karibuni kupitia sheria mpya ya uhalifu mtandaoni umetutia wasiwasi.

“Kama ujuavyo, mataifa washirika wa MCC wanapaswa kuendeleza na kuonyesha dhamira ya utawala bora, ambayo ni pamoja na kufuata misingi ya demokrasia na kulinda uhuru wa kutoa mawazo.

"Hata hivyo, matukio ya karibuni yanaifanya MCC na wadau wetu kujawa na maswali kuhusu dhamira hiyo,” inasomeka barua hiyo ya MCC iliyosainiwa na Bloom.

Kwa mujibu wa barua hiyo, MCC inafuatilia kwa karibu nyendo za Serikali katika ushughulikiaji wa masuala hayo ya utawala bora, hasa kipindi hiki kuelekea mkutano wa mwezi ujao wa bodi ya mfuko huo.

“Utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar kwa namna ya kuridhisha pande zote husika na haja ya kuiona Serikali ikifafanua hadharani nia yake na sheria ya uhalifu wa mtandaoni, kama vile kuchapisha utekelezaji wa kanuni zinazoakisi mchango wa mdau na kuonyesha dhamira ya kuendelea kulinda uhuru wa kutoa maoni, kutaisaidia MCC kuitathimini Tanzania kwa namna chanya juu ya kuendelea kwa dhamira yake ya kutimiza sharti la kufuzu kupata misaada,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ilimalizia kwa kusema: “Wasiwasi huu ni kikwazo cha mipango yetu ya ushirika. Tunaamini utashughulikia wasiwasi huu ipasavyo na tunatarajia kupata jibu kutoka kwako.”

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Likwelile, hakupatikana na hata alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea.

Pamoja na juhudi hizo, pia alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu, ambapo alipotafutwa Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, kuhusu barua hiyo ya MCC, alisema hana taarifa na hajaiona.

“Sina taarifa na wala sijaiona barua hiyo, hivyo siwezi kusema chochote labda mpaka nitakapoongea na bosi aniambie kama amepokea barua hiyo,” alisema Mduma.

Mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa nchini Marekani kuhudhuria shughuli za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN), alikutana na Mtendaji Mkuu wa MCC, Dana J. Hyde na watumishi waandamizi, akiwamo Makamu wa Rais wa Operesheni za mfuko huo, Kamran Khan.

Katika mkutano huo, MCC ilitangaza kuwa Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa awamu ya pili ya fedha za maendeleo kutoka katika mfuko huo, kuanzia mwakani, zaidi ya dola za Marekani milioni 472.8, sawa na zaidi ya Sh trilioni moja za Tanzania.

Katika mkutano huo, Rais mstaafu Kikwete, aliambatana na ujumbe wa maofisa kadhaa akiwamo Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Yusuf Omar Mzee.

Katika awamu ya kwanza ya fedha za MCC, Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 698 (sawa na Sh trilioni 1.46).

Kama MCC wataridhika na maelezo ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha, Tanzania itakuwa imepata jumla ya Sh trilioni 2.45 kwa awamu zote mbili kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka 10.

Awamu ya kwanza ya fedha hizo zilitumika kujenga Barabara za Tunduma- Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo- Songea- Mbinga.


Desemba 10, mwaka jana, Marekani pia ilibainisha hatua ya uamuzi wa utolewaji wa fedha za awamu ya pili za MCC utategemea hatua zitakazochukuliwa na Serikali kuhusu sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Uamuzi huo wa Marekani ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha nchini, ulionekana kama mtihani  wa pili kwa Rais mstaafu Kikwete, baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.

Waliowajibishwa na Rais Kikwete ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

Chanzo: Mtanzania
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Futa futa zote wakome na wizi wa kura CCM
    Waende kwa mabasha zao wachina na hao ndo wanaowapa jeuri
    EU pia futa futa misaada yote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahahah! Bado unaweweseka na uchaguzi sio........NDIO BASI TENA.....hata ikifutwa hiyo misaada, watakao-athirika ni CCM tu?? We'kweli CHIZI.....unafurahia, ndio kusema utahama nchi.........mfyuuuuuu

      Delete
    2. Chizi wewe Na CCM wote
      Mnategemea misaada kila kukicha
      Wakati mnafanya matanuzi kupita hata wanawotusadia
      Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

      Delete
    3. Uchumi mmekuwaliya

      Delete
    4. Uwiiiiiiiiiiiiiiiii,kumbe ndio maana Kagame alisema angekuwa na bandari umaskini kwenye nchi yake ingekuwa ndoto.AIBU KUBWA TANZANIA KWA KUHITAJI MISAADA TOKA NJE WAKATI TUNA UWEZO WA KUTOSHA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

      Delete
  2. NENO :UTAWALA BORA HESHIMA:UTAWALA BORA MAENDELEO:UTAWALA BORA.TUNAWASHUKURU SANA WATU WA MAREKANI KWA KUISAIDIA TANZANIA KIMAENDELEO KATIKA NYANJA LUKUKI TANGU TUJIPATIE UHURU.MISAADA HII NI PESA ZA WALIPA KODI WAMAREKANI AMBAO KIMSINGI WANAAMINI ULIBERALI.DEMOKRASIA YA KWELI,HAKI,UHURU WA MCHANGO WA MAWAZO,NA USHIRIKI SAWA KATIKA SIASA.SASA HIVI HAPA TANZANIA NA KWA MKONO WA KIKWETE MWENYEWE TULIFIKIA POORLY LOW YA 25%.HAPA HATUJAONA DALILI ZA GRAPH KUPANDA HATA CHEMBE.ESCROW.ZANZIBAR,MITANDAO,KAMATA WEKA NDANI.KWA UJUMLA DEMOKRASI YETU BADO SANA.KAMA MIAKA BASI 100 NYUMA.MCC MMETUBEBA SANA,HATUBEBEKI.

    ReplyDelete
  3. Sidhani kama Tanzania kwa sasa tunahitaji misaada, JPJM amesema hii nchi ni TAJIRI, hiyo misaada yenu ya masharti TUPA KULE............HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  4. HAO WALOKWEPA KODI NI ZAIDI YA HICHO KIASI CHA MSAADA CHENYE MASHARTI, WAKIBANWA HAKUNA HAJA YA MSAADA WA MTU, TUTAJITEGEMEA WENYEWE

    ReplyDelete
  5. Misaada ya masharti hatuitaki, tuko tayari kuishi kama Zimbabwe, Mugabe kiboko ya marekani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tupo ulaya inauma sana tunalipa kodi
      Tunasadia tz
      Kwasisi tunasadia ndugu zetu pia
      Bado CCM wanatesa kwa pesa zetu

      Delete
  6. Tuache ushabiki aomba mtoe mawazo chanya U-ccm na U-chadema hautupeleki mbali. Hii misaada ingetumika vizuri inasaidia ingawa kwa upande mwingine inalemaza, pia ukandamizaji wa sheria sio mzuri, mf. sheria ya mtandao inaathiri mawazo ya mtu. Sasa hivi hata kama unawazo nzuri unaogopa kutoa ukifikiri labda utakosea then utakamatwa. Pia hatutakuwa na uhuru wa kukosoa watawala wetu wala kutoa taarifa pindi utakapoona utata mahali. Naomba tuwe wakweli Tanzania tunaweza kama tukiwa kitu kimoja kwa kujiletea maendeleo. Tupokee misaada tutumie vizuri kama singapore ilivyofanya.

    ReplyDelete
  7. Sii kweli kama sheria ya mitandao imeathiri kitu, naona kiasi fulani imesaidia kuleta habari zisizokuwa na uhakika na nidhamu kwa kila mtu itarudi. Kama utachangia bila matusi wala uvumi nani akukamate? Tuichukie misaada na tuache itikadi za kichama tufanye kazi bure aghali jamani. Go Magufuli Mungu awe na wewe kutusaidia watanzania wote.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad