Masanja Mkandamizaji Achukua Form za Kugombea Ubunge Ludewa na Ktangaza nia Kuchukua Nafasi ya Marehemu Filikunjombe

Masanja Mkandamizaji
MSANII maarufu na mwigizaji Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la (Masanja mkandamizaji) ameahidi kuvaa viatu vya Deo H. Filikunjombe kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Ludewa na kusema ana uwezo mkubwa na kasi kama ya marehemu Filikunjombe ambaye alikuwa rafiki yake.

Ameyasema hayo alipokuja kuchukua fomu ya kugombea kupata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi,jumla ya watu tisa akiwemo mdogo wa marehemu Fillipo Filikunjombe ambaye ni mwanasheria wa TCRA wamechukua fomu ili kuweza kuomba ridhaa.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jitizame wewe unafikiri bungeni ni kuigiza watu

    ReplyDelete
  2. anaongeza umaharufu kwamba na yeye aliwahi kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge.

    ReplyDelete
  3. Hakuna kupeana nafasi kifamilia. CCM acheni hayo apewe anayefaa, Wee Masanja sasa nani atakuchukulia serious wakati hata mahubiri unayatoa kiutani? kweli bunge la tz limekosa hadhi ni comedy tu.,

    ReplyDelete
  4. huyu ana njaa ya pesa tu, hii nchi ni shamba la bibi aisee, kila anayetaka pesa za haraka haraka anakimbilia kwenye siasa!!

    ReplyDelete
  5. unaijua njombe na watu wake vizuri masanja?hawa watu wa njombe ni waelewa sana.najaribu kukuangalia masanja mgaya naona kama unaota vile,njozi njema.

    ReplyDelete
  6. Na bado ulichelewa wapi kama hutapata aibu ile iliyompata Yahaya (Davis Mosha(

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad